Zama za Giza
Mwanzo wa utawala wa Kanisa la Rumi ulikuwa mwanzo wa Zama za Giza. Kwa kadiri uwezo wa kanisa lile ulivyoongezeka, ndivyo na giza ilivyozidi kuwa nene. Imani ya watu ikatolewa kutoka kwa Kristo aliye msingi wa kanisa wa haki, wakamwadhimisha papa. Badala ya kumtegemea Mwana wa Mungu kwa kuzisamehe dhambi na kwa wokovu wa milele, watu wakamtazamia papa na maaskofu na makasisi ambao papa aliwapa mamlaka. Walifundishwa ya kwamba papa ndiye aliyekuwa mpatanishi wao mbele za Mungu, na ya kwamba hakuna awezaye kumkaribia Mungu isipokuwa kwa papa, tena ya kwamba papa alikuwa mahali pa Mungu kwao, na kwa hiyo alistahili kuheshimiwa na kusikiwa kabisa. Kukosa kumtii na kuyafanya mapenzi yake papa kulikuwa sababu ya mkosaji kupata adhabu kali ajabu mwilini na rohoni.VK 24.1
Hivi fikara za watu zikageuzwa toka kwa Mungu, ili wawaadhimishe wanadamu wakosaji na wakatili—naam, wakamheshimu mfalme wa giza mwenyewe, ambaye aliwaongoza na kuwatumia kwa kazi yake. Dhambi ilifunikwa na vazi la utakatifu. Maandiko Matakatifu yanapokataliwa, na mwanadamu anapoanza kujidhania kwamba yeye ndiye mkuu, hapo twaweza kutazamia ulagai, udanganyifu, na ufisadi. Kwa kuzikuza sana sheria na desturi za kibinadamu, ndipo ubaya wa kila namna ukatokea kwa ajili ya kuaclia kuzifuata amri za Mungu.VK 24.2