Uingereza na Scotland Zapata Nuru
Siku zile Luther alipokuwa akiwafungulia watu wa Ugermani Biblia ambayo ilikuwa imefungwa, Tyndale alivutwa na Roho wa Mungu kufanya vile kwa Uingereza. Alikuwa mwanafunzi wa Biblia mwenye bidii sana, na kwa ushujaa sana aliyahubiri mambo yote aliyosadikishwa kwamba ni ya kweli, akisema ya kwamba mafundisho yote yapate kuthibitika kwanza na Neno la Mungu. Juhudi yake haikuwa na budi kuleta ushindani kati yake na wafuasi wa Papa Mtaalamu fulani Mkatoliki aliyekuwa akishandana naye alisema hivi: “Laiti kama tungeishi bila sheria ya Mungu zaidi ya kukosa kuwa na amri za Papa.” Tyndale alimjibu akisema, “Namdharau sana Papa na amri zake zote; na Mungu akinihifadhi maisha, baada ya miaka si mingi nitamfanya kijana afanyaye kazi ya ukulima ayajue Maandiko Matakatifu kuliko uyajuavyo wewe.”VK 47.2
Kusudi aliloanza kuliweka moyoni, yaani kusudi la kuwapa watu Agano Jipya katika lugha yao wenyewe, sasa lilithibitika. na punde si punde alijitia katika kazi hiyo. Ilionekana ya kwamba alifungiwa pote katika Uingereza” naye aliona ni vema akimbilie Ugermani. Hapo akaanza kulichapa Agano Jipya katika Kiingereza. Baada ya muda si mrefu nakili elfu tatu za vitabu vya Agano Jipya vikamalizika, na katika mwaka ule ule, ikachapwa jumla ya nakili nyingine tena.VK 48.1
Hatimaye aliishuhudia imani yake kwa kuuawa, lakini silaha alizozitayarisha zimewawezesha askari wengine wa msalaba kupigana kwa kame nvingi mpaka siku hizi.VK 48.2
Shujaa aliyepatikana kwa kuitetea Injili katika nchi ya Scotland aliitwa John Knox. Mtu huyu wa haki hakumwogopa ye yote. Mioto ya mateso iliyowaka pande zake zote haikumtia hofu, bali ilizidi kumwongeza juhudi. Ingawa alikuwa katika hatari ya kuuawa alisimama imara, akijitahidi kwa uwezo wake wote apate kuiharibu ibada ya sanamu. Hivyo alishikilia kusudi lake, akipigana vita vya mwenyewe. Kila mfalme, mtawala, mwanasheria au mkuu Bwana, mpaka Scotland ikawa huru.VK 48.3
Katika Uingereza kulikuwa na mtu aitwaye Latimer, aliyehubiri kwenye mimbara akisema ya kwamba Biblia inapasa kusomwa katika lugha ya watu wenyewe. Alisema ya kwamba Mwenye kuanzisha Maandiko Matakatifu “ndive Mungu mwenyewe;” na haya Maandiko Matakatifu yana nguvu na uwezo wa kuishi milele kama alivyo Mungu mwenyewe. Kila mfalme, mtawala, mwanasheria au mkuu ye yote hana budi kulitii Neno takatifu la Mungu. “Tusiifuate njiayo yote nyingine, bali Neno la Mungu na Iituongoze; tusifuate njia za babu zetu, wala tusiyafuate matendo yao, lakini tufuate yale ambayo yaliwapasa kuyafanya.”VK 48.4
Barnes na Frith, waliokuwa rafiki waaminifu wa Tyndale, wao pia waliondoka wapate kuutetea ukweli. Watu walioitwa Ridley na Cranmer wakawafuata. Waongozi hawa wa Matengenezo katika Uingereza walikuwa watu walioelimika sana, na wengi wao walikuwa wakiheshimiwa sana kwa ajili ya juhudi yao na maisha ya utauwa katika Kanisa la Kirumi. Uasi wao kwa mamlaka ya Papa. Ujuzi wao juu ya siri za Babeli ulitilia uwezo zaidi kwa ushuhuda wao juu ya Babeli.VK 49.1
Fundisho kuu la akina Tyndale, Frith, Latimer, na Ridley ni ya kwamba maandiko yalitoka kwa Mungu, na ya kwamba ndani yake pana mafundisho yote yafaayo kwa wokovu. Mafundisho yao yalipinga kabisa ile desturi ya mapapa, baraza, makasisi na wafalme na kujitwalia nguvu za kuitawala dhamira ya watu juu ya mambo ya kiroho. Biblia ndiyo iliyokuwa kipeo cha wale watengenezaji, na mafundisho yao na madai yao yote waliyalinganisha na Biblia tu. Imani waliyokuwa nayo kwa Mungu na kwa neno lake ndiyo iliyowahifadhi watakatifu hawa walipoyatoa maisha yao kufa kama mashahidi kwa ajili ya imani ya dini.VK 49.2