Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Sita - Kushindwa Kuendelea

    *****

    KAZI ya Matengenezo ya dini haikukoma baada ya kufa kwa Luther, kama wengine wanavyodhani. Kazi hiyo itaendelea mpaka mwisho wa mambo ya dunia hii. Luther alikuwa na kazi kubwa sana kushirikisha wengine nuru aliyopewa na Mungu; walakini hakupokea nuru yote iliyopasa kutolewa kwa walimwengu. Tangu siku zile mpaka sasa, Maandiko Matakatifu yamekuwa yakiangazwa zaidi na zaidi kila mara, na mambo mengine ya ukweli yamekuwa yakizidi kufunuliwa mara kwa mara.VK 50.1

    Luther na watenda kazi wenzake walimfanyia Mungu kazi kubwa sana, lakini kwa jinsi wao wenyewe walivyotoka katika Kanisa la Kirumi, tena walikuwa wakiamini na kuyashuhudia mafundisho yake, haikuweza kutazamiwa ya kwamba wangeyatambua makosa haya yote. Ilikuwa kazi yao kuivunja minyororo ya Rumi na kutoa Biblia kwa walimwengu; walakini, kulikuwa na mambo makuu waliyoshindwa kuvumbua, tena makosa makubwa ambayo hawakuyakana. Wengi wao waliendelea kuitunza Jumapili pamoja na siku kuu zingine za Kirumi. Kwa kweli, hawakuitunza Jumapili wakifikiri ya kwamba ilikuwa siku takatifu ya Mungu, hali waliona ya kwamba inafaa kutunzwa kama siku ya kawaida ya ibada. Walakini, kulikuwa na wengine kati yao ambao waliiheshimu Sabato ya amri ya nne. Kati ya wale watengenezaji wa dini, inatupasa kuwaheshimu wale ambao walishuhudia kweli ambayo ilikuwa imedharauliwa, hata na Maprotestanti—yaani wale walioshikilia uthabiti wa amri ya nne na sharti ya Sabato ya Biblia. Matengenezo yalipofukuza mbali giza iliyokuwa imefunika nchi zote za Kikristo, watunza Sabato walipata kubainishwa katika nchi nyingi.VK 50.2

    Wale waliopata mibaraka mikubwa ya Matengenezo hawakuendelea mbele katika njia ile iliyofuatwa na Luther. Watu wachache waaminifu walitokea mara kwa mara kuyahubiri mambo mapya ya ukweli, na kuonyesha uongo uliokuzwa tangu zamani, lakini wingi wa watu, sawa na Wayahudi katika siku za Kristo, na wafuasi wa Papa katika siku za Luther, waliridhika wakaendelea kufuata mafundisho ya baba zao, na kuishi jinsi baba zao walivyoishi. Kwa hivyo dini ilianza kurudi nyuma kwa unafiki; makosa yalianza kukuzwa, pamoja na matendo yanayofuatana na kuamini mambo ya ushirikina, ambayo yangalitupwa mbali kama kanisa lingaliendelea kuenenda katika nuru ya Neno la Mungu. Hivi roho ile iliyoamshwa na Matengenezo ya dini, ilianza kufifia, mpaka Matengenezo makubwa yakahitajiwa katika makanisa ya Maprotestanti kama yalivyohitaji mwanzoni katika Kanisa la Kirumi katika siku za Luther. Kulikuwa na hali ya kuzimia maisha ya kiroho, na kuyakubali maoni ya wanadamu, hali ya kuipenda dunia, na kuyakubali mafundisho ya kibinadamu badala ya mafundisho ya Neno la Mungu. Kiburi na upotovu wa mali ulikuzwa kwa kuzifunika na kawaida za dini. Makanisa yaliingia katika upotovu kwa kushirikiana na dunia. Hivi mafundisho makuu yakashushwa ambayo kwa ajili yake Luther na watenda kazi wenzake walikuwa wametaabika sana.VK 51.1

    Shetani alipoona ya kwamba alishindwa kuivunja kabisa nguvu ya ukweli kwa njia ya mateso, alirudia tena azimio la mapatano ambalo mwanzoni lilileta uasi mkuu na kuanzishwa kwa kanisa la Kirumi. Aliwashawishi Wakristo wafanye urafiki, siyo sasa na wale washenzi, bali na wale ambao, kwa njia ya kumwabudu mungu wa dunia hii, wamejionyesha kweli ya kwamba ni waabuduo sanamu.VK 52.1

    Shetani hakuweza kuwanyima watu Biblia:kwa kuwa Biblia iliweza kununuliwa na watu wote. Lakini aliwadanganya watu maelfu wapate kuyakubali maelezo yake yasiyo ya kweli na mafundisho ya uongo, wasipochunguza Maandiko wao wenyewe ili wapate kujifunza ukweli; Shetani alikuwa ameyachafua mafundisho ya Biblia, na mazoea yalianza kuingia ambayo yangewaharibu watu milioni nyingi. Kanisa lilikuwa likiyashika na kuyatetea mazoea haya, badala ya kuishindania imani walivokabidhiwa watakatifu siku za kale. Na bila kujua hali yao na hatari yao, kanisa na watu wa dunia walikuwa wakikaribia wakati wa maana sana katika historia ya dunia—wakati atakapofunuliwa Mwana wa Adamu.VK 52.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents