Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Kumi Na Moja - Ujumbe Wa Malaika Wa Tatu

    *****

    KRISTO alipoingia katika patakatifu mno mbinguni ili kuifanya kazi ya mwisho ya upatanisho, aliwapa watumishi wake ujumbe wa mwisho wa neema, upate kutangazwa kwa watu wote wakaao duniani. Hilo ndilo onyo la malaika wa tatu lililoandikwa katika Ufunuo 14. Baada ya tangazo lile, mara nabii alimwona Mwana wa Adamu akija pamoja na utukufu wake apate kuyavuna mavuno ya dunia.VK 81.1

    Jinsi ilivyotabiriwa katika Maandiko, huduma ya Kristo katika patakatifu pa patakatifu ilianzishwa mnamo mwisho wa siku zilizotabiriwa, mwaka wa 1844. Maneno haya ya mwandishi wa Ufunuo yanahusika na wakati ule, “Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake.” Ufunuo 11:19. Sanduku la agano la Mungu liko katika sehemu ya pili ya patakatifu. Kristo alipoingia pale, kusudi kuhudumu kwa ajili ya mwenye dhambi, hekalu la . ndani lilifunguliwa, na sanduku la Mungu likaonekana. Utukufu na uwezo wa Mungu ulifunuliwa kwa wale ambao kwa imani walimwona Mwokozi akifanya kazi yake ya kuwaombea.VK 81.2

    Utukufu wake ulipolijaza hekalu, mwanga uliotoka katika patakatifu mno uliwaangazia watu waliokuwa waliinngoja duniani.VK 81.3

    Kwa imani, walikwisha kumfuata Kuhani wao Mkuu kutoka katika patakatifu mpaka patakatifu mno, na walimwona akiidai damu yake mbele ya sanduku la Mungu. Katika sanduku lile takatifu kuna sheria ya Baba, sheria ile iliyotolewa na Mungu mwenyewe kati ya ngurumo kule mlimani pa Sinai, na iliyoandikwa kwa mkono wake mwenyewe juu ya vibao vya mawe. Hakuna hata amri moja ambayo imetanguka; hakuna yodi wala nukta ambayo imegeuzwa. Mungu alipomtolea Musa nakala ya sheria yakei aliiweka sheria ya asili katika patakatifu mbinguni. Kwa kuzitazama amri zote moja moja, wale waliokuwa wakiitafuta kweli, katikati ya amri kumi waliiona amri ya nne ikiandikwa jinsi ilivyotangazwa mara ya kwanza: “Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. Siku sita utafanya kazi, utatenda mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala injakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako: maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba: kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato, akaitakasa.” Kutoka 20:8-11.VK 82.1

    Roho ya Mungu aliwavuta moyo wanafunzi hawa juu ya Neno lake. Walisadikishwa ya kwamba kwa kutojua kwao walikuwa wamekosea amri ya nne kwa ajili ya kutojali siku ya mapumziko ya Muumba. Walianza kuzichungua sababu za kuitunza siku ya kwanza ya juma badala ya siku ambayo Mungu aliitakasa. Hawakupata neno lo lote katika Maandiko Matakatifu lililowaonyesha ya kwamba amri ya nne ilikuwa imetanguka, wala hawakupata habari yo yote juu ya kugeuzwa kwa Sabato; baraka ile ya kuitakasa siku ya saba mwanzoni, ilikuwa haijaondolewa. Walikuwa wakitafuta kwa uaminifu sana ili wapate kujua na kuyafanya mapenzi ya Mungu, na walipofahamu ya kwamba walikuwa wamekosea sheria yake, mioyo yao ikajaa huzuni kuu. Mara wakaanza kuonyesha uaminifu wao kwa Mungu kwa kutunza Sabato yake takatifu.VK 82.2

    Watu wengi walijaribu sana kuipindua imani yao. Hakuna mtu ye yote aliyeshindwa kuona ya kwamba, kama patakatifu pa duniani palikuwa mfano wa patakatifu pa mbinguni, sheria iliyowekwa katika sanduku duniani ilikuwa nakili ya sheria iliyoko katika sanduku la mbinguni, na ya kwamba ikiwa mtu aliukubali ukweli juu ya patakatifu pa mbinguni, ilipasa kukubali na kuyatimiza madai ya sheria ya Mungu, pamoja na sharti ya amri ya nne juu ya Sabato.VK 83.1

    Wale ambao waiikubali fundisho juu ya kazi ya Kristo ya upatanishi, na umilele wa amri za Mungu> waiiona ya kwamba mambo haya ndiyo mafundisho yaliyodhihirishwa katika ujumbe wa malaika wa tatu. Malaika wa tatu asema, “Hapo ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Ufunuo 14:12. Maneno haya yametanguliwa na onyo lililo zito na la kutisha: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake.” Ufunuo 14:9,10. Maelezo yalitakiwa ili kudhihirisha wazi maana ya mifano iliyotumiwa hapa, kusudi kuufahamu ujumbe huu. Majina haya yalifananisha nini: mnyama.sanamu, na alama? Wale waliokuwa wakiutafuta ukweli wakarudia tena kujifunza maneno ya unabii.VK 83.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents