Kutakaswa kwa Patakatifu
Kwa jinsi dhambi za watu zilivyopitishwa. kwa mfano, mpaka patakatifu pa duniani kwa damu ya dhabihu ya dhambi, vivyo hivyo na dhambi zetu zinapitishwa mpaka patakatifu pa mbinguni kwa damu ya Kristo. Na kwa jinsi ambavyo kutakaswa kwa mfano kwa patakatifu pa duniani kulifanywa kwa kuondolewa kwa dhambi ambazo zilipachafua, vivyo hivyo na kutakaswa kuliko halisi kwa patakatifu pa mbinguni kutafanywa kwa kuondolewa, au kufutwa, kwa dhambi zilizoandikwa humo. Kufutiwa huku kwa dhambi kunataka ukaguzi wa vitabu, ili ionekane ya kwamba ni kina nani ambao, kwa kuzitubia dhambi na kumwamini Kristo, wanastahili kufadhiliwa na upatanisho wake. Kwa hivyo kazi ya kupatakasa patakatifu inafanya hukumu ya upelelezi kuwa ni lazima. Kazi hii ni lazima ifanywe kabla ya kuja kwa Kristo kuwaokoa watu wake, kwa kuwa atakapokuja, atakuja na ujira wake “kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” (Ufunuo 22:12.)VK 80.1
Kwa hivi wale waliofuata nuru iliyowatangulia katika maneno ya unabii, waiiona ya kwamba, badala ya kuja duniani mnamo mwisho wa siku 2,300 katika mwaka wa 1844, Kristo aliingia katika patakatifu mbinguni, usoni pa Mungu hasa, ili kuifanya kazi ya mwisho ya upatanisho, akiyafanya mambo tayari kwa kuja kwake.VK 80.2