Sura Ya Kumi Na Tatu - Madanganyifu Ya Shetani
*****
SHETANI alianzisha udanganyifu wake katika Edeni. Alimwambia Hawa, “Kufa hamtakufa.” Hapo ndipo Shetani alipoanza kufundisha ya kuwa mwanadamu ana hali ya kutokufa, na ameuendeleza udanganyifu huu tangu siku ile mpaka leo, tena atauendeleza mpaka siku ile Mungu atakaporejeza mafungo ya wateule wake. Nalionyeshwa Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Walitwaa tunda la mti ule uliokatazwa, ndipo upanga wa moto ukawekwa kuzunguka mti wa uzima, wakafukuzwa kutoka katika bustani, wasije wakalitwaa tena la mti wa uzima na kuwa wenye dhambi watakaoishi milele. Matunda ya mti huu yalikuwa na nguvu ya kudumisha hali ya kutokufa. Nalimsikia malaika fulani akiuliza hivi “Ni nani kati ya jamaa va Adamu ambaye ameupita upanga wa moto akalitwaa tunda la mti wa uzima?” Nilisikia malaika mwingine akijibu: “Hakuna hata mmoja wa jamaa ya Adamu ambaye ameupita ule upanga wa moto na kutwaa la mti wa uzima; hivyo hakuna mwenye dhambi aliye na hali ya kutokufa.” Roho ifanyayo dhambi itakufa milele—mauti ile ya mwisho ambayo baadaye hakuna kufufuka tena; ndipo ghadhabu ya Mungu itakwisha.VK 92.1
Mungu amesema, Roho ile ifanyayo dhambi, itakufa.” (Ezek. 18:4). Nalishangaa kuona jinsi Shetani alivyoweza kuwadanganya wanadamu hata waamini ya kwamba maana ya maneno haya ni kama kusema ya kwamba rohc ifanyayo dhambi haitakufa, bali itaishi milele katika maumivu makali. Malaika alisema, “Uzima ni uzima, ingawa ni kwa maumivu au furaha. Katika mauti hakuna maumivu, furaha, wala chuki.”VK 93.1
Shetani aliwaambia malaika zake wafanye bidii kuueneza ule uongo ambao kwao alimdanganya Hawa katika Edeni, akisema, “Kufa hamtakufa.7’ Na udanganyifu huu ulipokubaliwa na watu, wakiongozwa kuamini ya kwamba mwanadamu ana hali ya kutokufa, ndipo Shetani aliendelea kuwafanya kuamini ya kwamba miwenye dhambi ataishi katika maumivu ya milele. Ndipo njia ilipofunguliwa kwa Shetani na wajumbe wake kuwaonyesha watu ya kwamba Mungu ni mdhalimu mwenve kulipa kisasi, naye huwatupa katika Jehanum wale wasiompendeza na ya kwamba daima huwafanya waione ghadhabu yake; na wanapopata maumivu makali hivi, wakigaagaa katika moto wa milele, inasemwa ya kwamba Mungu huridhika moyoni akiwaona wakitaabika hivi. Shetani alijua ya kwamba kama watu wangekubali habari hii ya uongo, ndipo Mungu angechukiwa na wengi, badala ya kupendwa na kusujudiwa; tena wengine wengi wangefanywa kuamini ya kwamba maonyo ya Neno la Mungu yasingetimia kweli, kwani Mungu ni mkarimu mwenye upendo, na kuwapasha maumivu ya milele wale wanadamu aliokwisha kuwaumba kungekuwa tendo lililo mbali kabisa na tabia yake.VK 93.2
Jambo jingine la ajabu ni jinsi ambavyo Shetani amewafanya wanadamu waisahau kabisa haki ya Mungu na maonyo ya Neno lake na kusema ya kwamba Mungu ni mwenye neema, hata hakuna ye yote atakayepotea, bali wote, watakatifu na wenye dhambi, mwisho wataokolewa katika ufalme wake.VK 93.3
Kwa ajili ya mafundisho ya uongo juu ya hali ya wanadamu ya kutokufa, na juu ya maumivu yasiyo na mwisho, ambayo yanakubaliwa na wingi wa watu, Shetani aweza kuongoza watu wengine kusema ya kwamba Biblia haikutoka katika pumzi ya Mungu. Watu hawa huona ya kwamba Biblia inafundisha mambo mengi yaliyo mema, lakini hawawezi kuyasadiki maneno yake, kwa kuwa wamefundishwa ya kwamba Biblia hutangaza mafundisho ya maumivu ya milele.VK 94.1
Kuna watu wengine tena ambao Shetani huwapotosha zaidi, hata kuwafanya kusema ya kwamba Mungu hayuko. Hawaoni unyofu wa tabia zake zilivyoelezwa katika Biblia, kama anaweza kuwaletea watu wengine maumivu makali milele hata milele. Kwa hivyo watu hawa huikana Biblia na Mwandishi wake, na kusema ya kwamba kifo ni usingizi wa milele.VK 94.2
Tena kuna watu wengine ambao ni waoga, wepesi kutishwa. Shetani anawashawishi wapate kutenda dhambi, na wakisha kufanya dhambi, ndipo Shetani huwafanya kufikiri ya kwamba mshahara wa dhambi si mauti, bali ni kuishi katika maumivu makali ambayo hawana budi kuyavumilia milele na milele. Kwa kuwatangazia watu habari hii ya vitisho juu ya mahali zinapoadhibiwa roho za watu milele na milele, ndivyo Shetani anavyowapotosha watu, hata na kuwafanya wapotewe na akili zao. Hapo ndipo Shetani na malaika zake husimanga. tena makafiri na watu wasioamini ya kwamba Mungu yuko, wanashirikiana pamoja katika kulaumu dini ya Ukristo. Hudai ya kwamba mabaya haya ni matokeo ya kuiamini Biblia na Mwandishi wake, lakini kwa kweli yanatokea kwa ajili ya kusadiki mafundisho ya uongo yanayokubaliwa na wingi wa watu duniani.VK 94.3