Uchawi wa Namna ya Kisasa
Jina hasa la uchawi linadharauliwa siku hizi. Habari inayosema ya kwamba wanadamu wanaweza kuongea na pepo wachafu inafikiriwa kuwa hadithi ya Zama za Giza. Lakini imani hii juu ya kuongea na mizimu (yaani Spiritualism), inayofuatwa na watu maelfu, naam, watu milioni nyingi, na ambayo imepata nafasi ya Rupenya katika mambo ya elimu, na ambayo imeingia hata katika makanisa, tena inapendelewa na watu wa baraza kuu na katika majumba ya wafalme—udanganyifu mkubwa huu wa siku hizi sio jambo la kigeni hasa, lakini ni kuamsha kwa namna nyingine uchawi ule ule uliolaumiwa na kukatazwa katika siku za kale.VK 101.1
Shetani huwadanganya watu siku hizi kama vile alivyomdanganya Hawa katika bustani ya Edeni, kwa kuichochea tamaa ya kupata ujuzi isiyo halali yake. Shetani asema “Mtafumbuliwa macho nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Mwanzo 3:5. Lakini ujuzi unaoletwa na ile dini ya kuamini pepo ndiyo ile iliyosimuliwa na mtume Yakobo: “Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.” Yakobo 3:15.VK 101.2
Mkuu wa giza yu mwenye akili nyingi, naye huleta majaribu ya hila akigeuza majaribu na kuyafanyiza kufaa kwa kuwashika watu wa kila namna, wenye daraja na hali na uwezo mbali mbali. Hutumia “madanganyo yote ya udhalimu” ili kuwatawala wanadamu, lakini hawezi kuyatimiza mapenzi yake kwao ila tu kama wakikubali kushindwa na majaribu yake. Wale wanaojitia chini ya utawala wake kwa kuyaendeleza matendo yao mabaya na kukuza tabia zao zilizo mbaya, hawawezi kuufahamu mwisho wa mwenendo wao. Yule mwovu huwaharibu kabisa, ndipo huanza kuwatumia kwa kuwaharibu watu wengine pia.VK 101.3
Lakini hakuna ambaye liana budi kudanganywa na madai ya udanganyifu ya imani ya kuongea na mizimu (Spiritualism). Mungu ameutoa mwanga kwa walimwengu kutosha kuwadhihirishia madanganyo haya. Hata kama ushuhuda mwingine usingekuwako, kuna neno moja ambalo lingetosha Wakristo, ndilo linalosemwa ya kwamba pepo hawaweki tofauti yo yote kati ya wema na uovu, hata ya wanafunzi wanyofu wa Kristo na watumishi wabaya mno wa Shetani. Kwa Kuonyesha ya kwamba mtu aliye mwovu kabisa yuko mbinguni, na ya kwamba ameadhimishwa huko, kwa kweli ni kama Shetani huwatangazia walimwengu neno hivi: Haidhuru ukiwa mwovu wa namna gani; haidhuru kama unamwamini Mungu na Biblia au sivyo. Waweza kuishi maisha kama upendavyo; mbinguni makao yako.VK 102.1
Hata mitume, kama wakiigizwa na pepo hawa wa uongo, wanaonyeshwa kana kwamba wanayakanusha maneno waliyoyaandika kwa maongozi ya Roho Mtakatifu walipokuwa hapa duniani. Hukana ya kwamba Biblia ni Neno Takatifu la Mungu, na hivi huuondoa msingi wa tumaini la Wakristo na huizimisha taa inayoangaza njia iendayo mbinguni.VK 102.2
Shetani anawafanya walimwengu waamini ya kwamba Biblia ni kitabu cha hadithi zilizobuniwa tu, au ya kwamba ni kitabu kilichofaa kusomwa na mataifa ya zamani, lakini kwa sasa inafaa kuheshimiwa kidogo tu, ama kufikiriwa kuwa kitu cha zamani kisichotumika siku hizi. Na badala ya Neno la Mungu Shetani huleta maonyesho ya mizimu. Hapa ndipo njia inayokuwa chini ya utawala wake kabisa; kwa namna hii anaweza kuwafanya watu v aamini juu ya mambo yo yote apendavyo. Kile Kitabu kitakachomhukumu Shetani na wafuasi wake hukiweka gizani, kipate kudharauliwa jinsi atakavyo; na humfanya Mwokozi wa wanadamu asiwe na tofauti na mtu ye yote duniani. Na kama vile askari wa Kirumi waliolinda kaburi la Yesu walivyoeneza habari za uongo kama walivyoambiwa na makuhani na wakuu ili kuikanusha habari ya ufufuo wa Yesu, hivyo ndivyo ambavyo wale wanaoamini juu ya maonyesho ya mizimu wanavyowadanganya watu ya kwamba hakuna mambo ya ajabu wala mwujiza katika maisha ya Mwokozi wetu. Baada ya kumdharau Yesu hivi, huanza kuwatazamisha watu miujiza yao wenyewe wakisema ya kwamba miujiza hii huishinda ile iliyofanywa na Kristo.VK 102.3
Nabii Isaya asema hivi: “Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” Isaya 8:19, 20. Kama wanadamu wangekubali kuupokea ukweli unaoelezwa dhahiri katika Biblia, ya kwamba wafu hawajui kitu, ndipo wangeweza kuyaona maneno na maonyesho ya pepo kwamba ni kutenda kwake Shetani kwa uwezo na ishara na ajabu za uongo. Lakini kwa kuwa ni vigumu kwao kuacha kufuata mapenzi yao ya nia ya mwili, wasitake kujitenga na dhambi ambazo wanapendar kuzifanya, wingi wa watu wameyafumba macho yao wasione nuru; tena wanaendelea mbele bila kujali maonyo, wakati Shetani anapoweka tanzi lake la kuwategea, hao nao hushikwa naye. “Kwa sababu hawakubali kuipenda ile kweli. wapate kuokolewa,” kwa hiyo “Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo.” 2 The. 2:10, 11.VK 103.1
Wale wanaoyakataa mafundisho juu ya kuongea na mizimu (Spiritualism), si kwamba wanashindana na wanadamu tu, bali wanashindana na Shetani mwenyewe na malaika zake. Wameingia katika vita juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza la ulimwengu huu, na juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Shetani hataacha nafasi hata kidogo asipofukuzwa na uwezo wa wajumbe watokao mbinguni. Inawapasa watu wa Mungu kuwa tayari kumkabili kama Mwokozi wetu alivyomkabili na maneno haya, “Imeandikwa.” Hata sasa Shetani anaweza kuyataja mafungu ya Biblia kama alivyofanya katika siku za Kristo, naye atayageuza vibaya mafundisho ya Biblia ili yapate kulingana na madanganyifu yake. Lakini maneno yaliyoandikwa dhahiri katika Biblia yanakuwa silaha za kutosha kushinda katika kila shindano.VK 104.1
Wale ambao watasimama imara katika siku za taabu, inawapasa kufahamu ushuhuda wa Maandiko juu ya hali ya wanadamu na hali ya wafu jinsi ilivyo, kwa kuwa baada ya siku si nyingi watu wengi watafikiwa na pepo za mashetani wanaojifanya kuwa ni jamaa zao au rafiki zao waliokufa, wakiwatangazia mafundisho mabaya ya uzushi. Roho hizi za mashetani watatuvuta roho kwa kutuonyesha na kutuambia mambo ambayo tunajishughulisha nayo, na watafanya miujiza ili kuyathibitisha madanganyifu yao. Inatupasa kuwa tayari kuwashinda kwa ukweli wa Neno la Mungu ya kwamba wafu hawajui kitu, na ya kwamba wale wanaojitokeza hivyo hi roho za mashetani.VK 104.2
Kwa muda mrefu sana Shetani amekuwa akijitayarisha kwa jitihada yake ya mwisho kwa kuwadanganya walimwengu. Msingi wa udanganyifu wake uliwekwa na maneno hayo aliyomwambia Hawa: “Hakika hamtakufa. . . . siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Mwanzo 3:4, 5. Punde kwa punde ameitayarisha njia yake kwa kazi hii kuu kwa kuaminisha watu juu ya kuongea na mizimu. Hajayatimiza maazimio yake yote bado; lakini atayatimiza katika siku za mwisho kabisa. na wanadamu watatumbukizwa katika mambo haya ya udanganyifu. Kwa upesi sana watu wanatulizwa roho ya kwamba wa salama, na huku wako hatarini; lakini hawataamshwa ila na mmiminiko wa ghadhabu ya Mungu.VK 105.1