Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuja Kwa Kristo Katika Mwili

    Fundisho la uongofu wa ulimwengu na utawala wa kiroho Wakristo halikushilikiwa na kanisa la mitume. Kwa ujumla halikukubaliwa na Wakristo mpaka mwanzoni mwa kame ya kumi na nane. Lilifundisha watu kuutarajia ujio wa Bwana miaka mingi baadaye na liliwazuia wasiziangalie dalili zinazotangaza ukaribu wa marejeo yake. Liliwafanya wengi wadharau maandalizi ya kukutana na Bwana wao.TK 207.1

    Miller aligundua kuwa kuja kwa Kristo ni halisi na atakuja katika mwili kama ilivyofundishwa wazi katika Maandiko. “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu.” “Nao watamwona Mwana wa Mungu akishuka pamoja na mawingu ya mbinguni kwa nguvu na utukufu mwingi.” “Kama umeme utokavyo mashariki na kumulika hata magharibi; hivyo ndivyo atakavyokuja Mwana wa Adamu.” “Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wake pamoja na malaika zake.” Naye atatuma malaika zake pamoja na sauti ya tarumbeta nao watawakusanya watakatifu wake.” 1 Wathesalonike.4:16,17; Mathayo 24:30,27; 25:31; 24:31.TK 207.2

    Wakati wa kuja kwake, wenye haki waliokufa watafufuliwa na wenye haki walio hai watabadilishwa. “Hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.”. “Waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza: kisha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja mawinguni, ili tumlaki Bwana hewani: hivyo tutakuwa na Bwana milele” 1 Wakorintho 15:51-53; 1 Wathesalonike 4:16-17.TK 207.3

    Mwanadamu katika hali yake ya sasa, anafikwa na mauti, ni wa kuharibika; lakini ufalme wa Mungu hautakuwa wa kuharibika. Hivyo mwanadamu katika hali yake ya sasa, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Yesu atakapokuja, atawatunukia watu wake hali ya kutokufa, na kuwakaribisha waurithi ufalme ambao hata sasa wao ni warithi peke.TK 207.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents