Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Agano Jipya kwa Lugha ya Kifaransa

  Lakini wasingeweza kuyafikia matumaini yao. Majaribu na mateso vilikuwa vikiwangojea mitume wa Yesu. Hata hivyo wakati wa amani ulikuja, ili waweze kupata nguvu za kukabiliana na kimbunga kilichokuwa mbele yao, na Matengenezo yalisonga mbele haraka. Lefevre alichukua jukumu la kutafsiri Agano Jipya; ni wakati huo Luther alipotua, kutoka mitamboni, Biblia ya Kijerumani kule Wittenberg, Agano Jipya kwa lugha ya Kifaransa lilichapwa pale Meaux. Baada ya muda mfupi, wakulima wa Meaux walikuwa na Maandiko Matakatifu mikononi mwao. Wafanyakazi kwenye mashamba, na mafundi kwenye karakana zao, walijipa moyo katika kazi zao ngumu za kila siku kwa kuzungumzia ukweli wa thamani wa Biblia. Ijapo walikuwa ni watu wa daraja la chini sana, wasio na elimu na wakulima wadogo wadogo wafanyao kazi zao kwa bidii, uwezo wa neema ya Mungu wa kubadilisha na kuinua juu ulionekana katika maisha yao.TK 138.2

  Nuru iliyokuwa imewashwa Meaux ilitupa miali yake mbali. Idadi ya waongofu ilikuwa inaongezeka kila siku. Kwa kipindi fulani hasira isiyo na mipaka ya watawala ilizuiliwa na mfalme, lakini hatimaye utawala wa Papa ulishinda. Mti wa kuchomea watu ulisimamishwa tena. Wengi walishuhudia ukweli ndani ya miali ya moto.TK 138.3

  Katika kumbi za majumba ya kifahari na ikulu kulikuwa na wana na mabinti wa kifalme waliouthamini ukweli kuliko utajiri, cheo, ama hata maisha yenyewe. Louis de Berquin, alikuwa amezaliwa kwenye nyumba ya kiungwana, alijitoa kujifunza, huku akiwa amelelewa vizuri na mwenendo safi, mtu asiye na lawama yoyote kimaadili “aliamua kuupamba uaminifu wake wote kwa kuupokea Ulutheri kwa chuki ya pekee.” Kwa nguvu za Mungu aliongozwa kusoma Biblia, na alichokikuta kule “si mafundisho ya Kanisa la Roma bali mafundisho ya Luther.” Alijitoa kwa ajili ya Injili.TK 138.4

  Wafuasi wa Kanisa Katoliki nchini Ufaransa walimtupa gerezani kama “mwasi”, lakini mfalme alimwachia huru. Kwa miaka mingi, Francis alikuwa anatanga tanga kati ya Roma na Matengenezo. Berquin alifungwa mara tatu na mamlaka za utawala wa Papa, na kuachiwa huru na mfalme aliyekuwa amekataa kumtoa mhanga kwa sababu ya chuki za watawala. Kwa kurudia rudia, Berquin alikuwa ameonywa kuhusu hatari iliyokuwa inamkabili nchini Ufaransa na walimsihi afuate nyayo za wale waliokuwa wamepata hifadhi na kuwa wakimbizi kwa hiari yao.TK 139.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents