Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Malaika Walinzi

  Malaika mlinzi amewekwa kwa kila mfuasi Wakristo. “Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.” Akizungumza na wale wanaomwamini Mwokozi alisema: “malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.” Zaburi 34:7; Mathayo 18:10. Watu wa Mungu wakiwa wamefunuliwa mbele ya uovu usiolala wa mkuu wa giza, wanahakikishiwa ulinzi usiokoma wa malaika. Uhakika huo unatolewa kwa sababu wapo mawakala wenye nguvu kwa ajili ya kukabiliana nao- mawakala wasio na idadi, waliodhamiria na wasiochoka.TK 316.1

  Roho waovu, mwanzo waliumbwa bila dhambi, walikuwa na asili moja, uwezo, na utukufu kama viumbe watakatifu ambao sasa ni wajumbe wa Mungu. Lakini wakiwa wameanguka dhambini, walijiunga pamoja kwa ajili ya kumvunjia Mungu heshima na kuwaangamiza wanadamu.Waliungana na Shetani katika uasi, walishirikiana kupigana vita dhidi ya mamlaka ya Mungu.TK 316.2

  Historia ya Agano la Kale inataja uwepo wao, lakini wakati Kristo alipokuwepo duniani, roho waovu walionesha uwezo wao kwa hali ya juu zaidi. Kristo alikuja kumkomboa mwanadamu, na Shetani aliazimia kuudhibiti ulimwengu. Alikuwa amefaulu kuanzisha ibada ya sanamu katika kila sehemu ya dunia isipokuwa Palestina. Yesu alikuja akiinyosha mikono yake ya upendo kwa nchi ambayo ilikuwa haijajitoa kikamilifu kwa mjaribu, akiwaalika wote wapate msamaha na amani ndani yake. Majeshi ya giza yalifahamu kwamba endapo utume Wakristo ungefanikiwa, utawala wao ungekwisha mapema.TK 316.3

  Imeelezwa wazi katika Agano Jipya kwamba wanadamu wamekuwa wakipagawa na maShetani. Watu hao waliokuwa wakiteseka hawakuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa asili pekee; Kristo alitambua uwepo wa moja kwa moja wa mawakala wa roho waovu. Waliokuwa wamepagawa na pepo katika nchi ya Wagerasi, walikuwa wagonjwa, wakifurukuta, wakitoa povu, wakipiga kelele za fujo, walikuwa wanajifanyia vumgu wao wenyewe na kuhatarisha usalama wa wote ambao wangewasogelea. Miili yao iliyokuwa imelowa damu na akili zilizochanganyikiwa viliwakilisha kioja kilichokuwa kinamfurahisha mkuu wa giza. Mmoja wa maShetani aliyekuwa anawadhibiti waliokuwa wanateseka akanena kwa nguvu, “Jina langu ni Legioni: maana tuko wengi” Marko 5:9. Katika jeshi la Warumi legioni ilijumuisha watu kati ya 3,000 hadi 5,000. Kwa amri ya Yesu roho wachafu waliwatoka wale wahanga wao, wakiwaacha wakiwa wamepungua nguvu, wenye akili timamu, na waungwana. Lakini pepo waliwasomba kundi la nguruwe hadi baharini, na kwa wakazi wa nchi ya Wagerasi hasara waliyopata ilikuwa inazidi baraka Kristo alizokuwa amezitoa: Mungu mponyaji alikuwa ameamriwa kuondoka. Angalia Mathayo 8:22-34. Kwa kumtumpia Yesu lawama kwa hasara yao, Shetani aliamsha hofu za watu na kuwazuia kusikiliza maneno yake.TK 316.4

  Kristo aliruhusu pepo wachafu kuwaangamiza wale nguruwe kama karipio kwa Wayahudi waliokuwa wanafuga wanyama najisi kwa ajili ya biashara. Kama Yesu asingewadhibiti, wale pepo wangewaangamiza si nguruwe pekee bali pia waangalizi na wamiliki wao.TK 317.1

  Zaidi ya hayo,tukio hili liliruhusiwa ili wanafunzi wa Yesu washuhudie ukatili wa Shetani kwa wanadamu na kwa wanyama, ili wasidanganywe kwa mbinu zake. Yalikuwa ni mapenzi yake pia kuwa watu waweze kutazama nguvu yake ya kuvunja utumwa wa Shetani na kuwafungulia mateka wake. Ingawa Yesu mwenyewe aliondoka, yule mtu aliyekuwa ameokolewa kimuujiza alibaki ili atangaze rehema za mfadhili wao.TK 317.2

  Matukio mengine yameandikwa: Binti wa mwanamke Msirofoinike, akiwa amehuzunika na kuchukizwa na Ibilisi, ambaye Yesu alimtoa kwa njia ya Neno lake. (Marko 7:26-30); kijana aliyekuwa amepagawa ambaye mara nyingi, “amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize” (Marko 9:17-27); aliyepagawa, ameteswa na roho wa ibilisi mchafu aliyevuruga utulivu wa Sabato kule Kapemaumu (Luka 4:33-36)-—wote waliponywa na Mwokozi. Karibu katika kila tukio, Kristo alikuwa anazungumzia pepo kama kiumbe chenye akili, akimwamum kutomtesa yule mtu tena. Waabuduo huko Kapemaumu, “Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamum pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36.TK 317.3

  Kwa malengo ya kupata nguvu za miujiza, Baadhi ya watu walikuwa wanakaribisha mivuto ya kishetani. Hiyo haikupingana na maShetani. Miongoni mwa watu wa kundi hili ni wale waliokuwa na roho wa uaguzi- Simon Magus, Elima mchawi, na kijakazi aliyewafuata Paulo na Sila kule Filipi, Angalia Matendo. 8:9, 18; 13:8; 16:16-18.TK 318.1

  Hakuna watu walio katika hatari kubwa kama wale wanaokataa uwepo wa ibilisi na malaika zake. Wengi huzingatia rai zao huku wakijidhania kuwa wanafuata hekima yao wenyewe. Kwa kadiri tunavyokaribia kufungwa kwa wakati, Shetani anatumia nguvu kubwa zaidi kudanganya, anasambaza kila mahali imani kwamba yeye hayupo. Ni sera yake kujificha mwenyewe na utendaji kazi wake.TK 318.2

  Mdanganyifu mkuu anaogopa kuwa tutazifahamu mbinu zake. lli kuificha tabia yake halisi anajifanya mwenyewe aonekane kama kitu cha kudhihakiwa au kutwezwa. Anafurahia anapochorwa na kuonekana kama mpumbavu, mwenye umbile baya, nusu mnyama na nusu mtu. Anafurahia kuona jina lake likitumiwa kwenye michezo na mizaha. Kwa sababu amejificha mwenyewe kwa ujuzi kamili, swali linaloulizwa mara nyingi: “Je, kiumbe wa aina hiyo yupo?” Shetani ana uwezo wa kudhibiti kwa upesi mioyo ya wale ambao hawafahamu juu ya mvuto wake. Neno la Mungu linafunua mbele zetu nguvu zake za siri,na hivyo kutuweka sisi katika hali ya kuwa macho.TK 318.3

  Tunaweza kupata kimbilio na ukombozi katika nguvu kubwa ya Mwokozi wetu. Kwa uangalifu tunafunga milango yetu kwa komeo na kufuli ili kulinda mali zetu na maisha yetu dhidi ya watu waovu, ni mara chache tunafikiria juu ya malaika waovu ambao mashambulizi yao hatuna nguvu zetu wenyewe kujilinda nayo. Kama wakiruhusiwa wanaweza kuzivuruga akili zetu, kuiletea maumivu miili yetu, kuharibu mali zetu na maisha yetu. Lakini wale wanaomfuata Kristo wako salama chini ya uangalizi wake. Malaika wenye nguvu nyingi wanatumwa kuwalinda. Yule mwovu hawezi kupita ulinzi ambao Mungu ameuweka kwa watu wake.TK 318.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents