Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 7 - Luther, Mwanamume Kwa Wakati Wake

    Mtu wa kwanza miongoni mwa wale walioitwa kuliongoza kanisa litoke kwenye giza la utawala wa Papa liingie kwenye nuru safi ya imani alikuwa Martin Luther. Hakuwa na hofu na chochote isipokuwa kicho kwa Mungu. Hakutambua msingi mwingine wa imani isipokuwa Maandiko Matakatifu. Luther alikuwa ni mwanamume wa enzi zake.TK 78.1

    Luther alitumia miaka yake ya awali katika nyumba duni ya mkulima wa Kijerumani. Baba yake alikuwa amedhamiria Luther awe mwanasheria, lakini Mungu alikuwa amekusudia kumfanya mjenzi wa hekalu lililokuwa linainuka taratibu kwa kame nyingi. Taabu, upweke, na adhabu kali ilikuwa ni shule iliyotumiwa na Mungu kumwandaa Luther kwa ajili ya Utume maishani mwake.TK 78.2

    Baba yake Luther alikuwa mtu mwenye akili ya utendaji. Hisia zake bora zilimwongoza kuutilia mashaka mfumo wa maisha ya kitawa. Hakufurahishwa na Luther ambaye, bila idhini yake alikuwa ameingia katika nyumba ya watawa. Ilipita miaka miwili kabla baba hajafanya mapatano na kijana wake, na baada ya hapo nia yake haikubadilika.TK 78.3

    Wazazi wa Luther walijitahidi kumfundisha mtoto wao katika kumjua Mungu. Jitihada zao zilikuwa za dhati na za kudumu kuwaandaa watoto wao kwa maisha yenye manufaa. Wakati fulani walifanya kwa ukali sana, lakini Mwanamatengenezo huyu alipata mafundisho zaidi katika adhabu zao kuliko shutuma.TK 78.4

    Shuleni, Luther alikuwa anatendewa kwa ukali na hata kwa ukatili. Wakati mwingi aliteseka kwa njaa. Mawazo ya dini yaliyojengwa kwenye huzuni na mapokeo potuvu yaliyokuwepo nyakati hizo yalimjaza kwa hofu. Angeweza kulala usiku akiwa na moyo wa huzuni, na hofu ya kudumu alipomwazia Mungu kuwa ni katili na dhalimu, badala ya Baba mwema wa mbinguni.TK 78.5

    Alipoingia katika Chuo Kikuu cha Erfurt, matarajio yake yaling’aa zaidi kuliko ilivyokuwa kwenye miaka ya awali. Wazazi wake, kwa kujibana na kazi nyingi waliweza kumtimizia mahitaji yote yaliyokuwa yanatakiwa. Na marafiki waliokuwa waangalifu kwake walipunguza madhara ya huzuni katika mafunzo yake ya awali. Kwa njia ya mivuto inayofaa, akili yake ilikua kwa haraka. Kutumika kwake bila kuchoka, mapema, kulimweka nafasi ya juu miongoni mwa rafiki zake.TK 78.6

    Luther hakuacha kuianza siku kwa sala, moyo wake ulidumu katika maombi kwa ajili ya uongozi wa Mungu. Mara nyingi alisema, “Kuomba vema ni nusu ya kujifunza vizuri” 35D’Aubigne, bk. 2, ch. 2.TK 79.1

    Siku moja aligundua Biblia kwenye maktaba ya Chuo Kikuu, kitabu ambacho hakuwahi kukiona. Aliwahi kusikia sehemu tu za Injili na Nyaraka, ambazo alidhani kuwa ndiyo Biblia nzima. Sasa, kwa mara ya kwanza, aliliangalia Neno zima la Mungu. Kwa kicho na mshangao alizifungua kurasa takatifu na kuyasoma mwenyewe maneno ya uzima, akipumzika na kuonesha mshangao, “Oo kwamba Mungu angenipa kitabu kama hiki kwa ajili yangu!” 36Ibid Malaika walikuwa kando yake. Miali ya nuru kutoka mbinguni ilifunua hazina za ukweli kwenye ufahamu wake. Hatia ya kina juu ya hali yake kama mwenye dhambi ilimshika kuliko wakati mwingine kabla.TK 79.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents