Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Enzi ya Hofu Kuu

    Maskini wafuasi wa imani ya Wanamatengenezo waliokuwa wamezoea kuwakusanya waumini kwenye maeneo yao ya kukutania ya siri walikamatwa. Kwa tishio la kuua palepale kwenye nguzo ya kuchomea watu moto, mfalme aliagizwa kufanya kazi kama balozi wa Papa katika kila nyumba ya Mprotestanti pale mjini. Hofu ya moto ilitawala, mfalme alikuwa ameridhia kuwasaliti ndugu zake. Mpelelezi wa mfalme aliyekuwa anaitwa Morin, akifuatana na msaliti, kimya kimya na polepole alikuwa anapita kwenye mitaa ya mji. Alipofika mbele ya nyumba ya Mlutheri, msaliti alikuwa anaonesha ishara, bila kutamka neno lolote. Msafara ulisimama, waliingia kwenye nyumba na watu wa familia ile wakiburutwa na kufungwa minyororo na msafara huu wa kutisha uliendelea mbele kuwasaka wahanga wengine wapya. “Morin aliufanya mji utetemeke...ilikuwa ni enzi ya hofu kuu.” 140lbid. bk. 4, ch. 10.TK 144.3

    Wahanga waliuawa kwa mateso makali, ilikuwa imeagizwa ya kwamba moto upunguzwe kuwaka kwake ili kurefusha muda wa maumivu yao. Wao walikufa kama washindi, uvumilivu na uaminifu wao haukutikiswa, amani yao ilikuwa angavu. Watesi wao walihisi kuzidiwa nguvu. “Paris yote iliwezeshwa kuona aina gani ya watu dhana mpya inaweza kuwatengeneza. Hakukuwa na mimbari kama rundo la kuni za kuchomea wafia dini. Furaha iliyotulia iliangaza kwenye nyuso za watu hawa walipokuwa wakipita... kwenda mahali pa kuuawa kwao...walikuwa wanasihi kwa sauti isiyoweza kupingwa kwa niaba ya Injili.” 141Wylie, bk.l3,ch. 20.TK 145.1

    Waprotestanti walishtakiwa kwa kupanga kuwaua Wakatoliki kinyama, kuipindua serikali na kumwua mfalme. Hakukuwa na chembe yoyote ya ushahidi uliotolewa kuthibitisha tuhuma hizo. Lakini, bado ukatili waliokuwa wanatendewa Waprotestanti wasio na hatia, vilikuwa vinaendelea kurundikana na kuongeza uzito wa adhabu, na kame zitakazofuata zingeleta maangamizi waliyokuwa wameyatabiri, juu ya mfalme, serikali na watu wake. Maangamizi hayo yaliletwa na makafiri na wafuasi wenyewe wa Ukatoliki. Kukandamizwa kwa Uprotestanti kungeiletea Ufaransa maafa haya makubwa.TK 145.2

    Wasiwasi, kutoaminiana, na hofu vilikuwa vimeenea kwenye daraja zote za jamii. Mamia walikimbia kutoka Paris, wakimbizi walioondoka nchi ya kwao kwa matashi yao wenyewe, kwa sehemu kubwa wakitoa tangazo la kwanza kwamba walikuwa wanapendelea imani ya matengenezo. Wafuasi wa Kanisa Katoliki walikuwa wanawaangalia watu hawa kwa mshangao mkubwa kwa dhana kwamba walikuwa “waasi” ambao hawakuwashuku na ya kuwa walikuwa wanavumiliwa miongoni mwao.TK 145.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents