Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 26 - Watetezi Wa Ukweli

    Matengenezo ya Sabato katika siku za mwisho yalitabiriwa katika kitabu cha Isaya: “Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye Sato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote...Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye Sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.” Isaya 56:1, 2, 6,7.TK 281.1

    Utendaji wa maneno haya upo katika zama za Ukristo kama inavyooneshwa kwenye muktadha (soma fungu la 8). Hapa umetabiriwa mkusanyiko wa mataifa kwa ajili ya Injili, wakati watumishi wa Mungu wanapohubiri habari ya furaha kwa kila taifa.TK 281.2

    Bwana aliamuru, “...ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu.” Muhuri wa Mungu unapatikana kwenye amri ya Nne. Amri hii pekee, kati ya kumi, huonesha jina na cheo cha Mtoa sheria. Wakati Sabato ilipobadilishwa na mamlaka ya Papa, muhuri ulitolewakutoka kwenye sheria. Wanafunzi wa Yesu wanaitwa kuurejesha muhuri kwa njia ya kuiinua Sabato kama kumbukumbu ya Mwumbaji na alama ya mamlaka yake.TK 281.3

    Amri imetolewa: “Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao.” Wale ambao Mungu anawaita, “Watu wangu” watashutumiwa kwa ajili ya dhambi zao, na daraja la watu wanaojidhania kuwa ni wenye haki katika kumtumikia Mungu. Karipio hili zito la Yule anayeichunguza mioyo ni uthibitisho kuwa wanaoyakanyaga maagizo ya Mungu. Isaya 58:1, 2.TK 281.4

    Kwa hiyo nabii anaionesha sheria iliyoachwa: “utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia. Kama ukigeuza mguu wako usihalifu Sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita Sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika Bwana.” Isaya 58:12-14.TK 282.1

    Mahali “palipobomoka” katika sheria ya Mungu ni badiliko la Sabato lililofanywa na mamlaka ya Kirumi. Lakini muda umefika wa kutengeneza mahali palipobomoka.TK 282.2

    Sabato ilikuwa inashikwa na Adamu alipokuwa hana hatia pale Edeni; Adamu alikuwa anaishika baada ya anguko, akiwa ametubu baada ya kufukuzwa kutoka kwenye shamba lake. Ilikuwa inashikwa na wazee wote kuanzia Habili hadi Nuhu, hadi Ibrahimu, hadi Yakobo. Alipokuwa amewakomboa wana wa Israeli, Mungu aliitangaza sheria yake kwenye makutano.TK 282.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents