Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Masharti Vamewekwa Bayana

    “Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure” Ahadi hii ni kwa wale tu wenye kiu. “Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.” Ufunuo 21:6,7 Masharti yamebainishwa. Ili kupata urithi wa vitu vyote ni lazima tuishinde dhambi.TK 331.1

    “Haitakuwa heri kwa mwovu” Mhubiri 8:13. Mwenye dhambi anajiwekea mwenyewe, “akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu; atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake, “dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu.” Warumi 2:5, 6, 9.TK 331.2

    “Hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme Wakristo na Mungu.” “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.” Waefeso 5:5; Ufunuo 22:14, 15TK 331.3

    Mungu amewapa wanadamu tamko juu ya kanuni yake ya kushughulikia dhambi. “Na wote wasio haki atawaangamiza.” “Wakosaji wataangamizwa pamoja, Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.” Zaburi 145:20; 37:38. Mamlaka ya serikali ya Mungu itakomesha uasi, lakini adhabu ya haki italingana na tabia ya Mungu, mwenye rehema na ukarimu.TK 331.4

    Mungu hashurutishi dhamiri. Mungu hapendezwi na utii wa kitumwa. Anatamani kwamba viumbe walio kazi ya mikono yake wampende kwa sababu anastahili upendo. Anawataka wamtii Yeye kwa sababu wana akili ya kuitambua hekima yake, haki, na ukarimu wake.TK 331.5

    Kanuni za serikali ya mbinguni zinapatana na agizo la Mwokozi, “Wapendeni adui zenu” Mathayo 5:44. Mungu huwatendea haki waovu kwa faida ya ulimwengu na hata kwa manufaa ya wale ambao hukumu yake inawaangukia. Anaweza kuwapa furaha akipenda. Anawazingira kwa thawabu za upendo wake na anawafuata akiwapa rehema; lakini wanalipuuza pendo lake, wakiibatilisha sheria yake, na kuitupa rehema yake. Daima wakipokea vipawa vyake, hawamheshimu mtoaji. Mungu anauvumilia ukaidi wao kwa muda mrefu; lakini je, atawafunga pingu waasi hawa ili wawe upande wake na kuwalazimisha kutenda mapenzi yake?TK 331.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents