Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Waliokombolewa Wakiwa Kwenye Utukufu

    Katika zama zote wateule wa Bwana wamekuwa wakitembea katika njia nyembamba. Walitakaswa katika tanuru la mateso. Kwa ajili ya Yesu walivumilia kuchukiwa, kusingiziwa, kujikana nafsi, na kukatishwa tamaa. Walijifunza ubaya wa dhambi, nguvu yake, hatia yake, huzuni yake, wanaiangalia kwa chuki. Kutambua jinsi kafara ya milele ilivyotolewa ili kuondoa tatizo la dhambi kunawafanya wajishushe na kunaijaza mioyo yao shukrani. Wanapenda zaidi kwa sababu wamesamehewa dhambi nyingi zaidi. Angalia Luka 7:47. Washirika wa mateso ya Kristo, wanastahili kuwa washirika wa utukufii.TK 388.2

    Warithi wa Mungu watatokea katika upenu, vibanda vibovu, magereza ya chini ya ardhi, majukwaa ya kunyongea wahalifu, milimani, katika majangwa, mapango. “Walikuwa maskini, walinyanyaswa, waliteswa.” Mamilioni walikwenda kaburini kwa kusingiziwa mabaya kwa sababu walikataa kukubaliana na Shetani. Lakini sasa hawateswi tena, kutawanywa na kukandamizwa. Kutoka sasa watasimama wakiwa wamevikwa mavazi mazuri kupita mavazi ambayo matajiri walioheshimika duniani waliwahi kuvaa, wakiwa wamevikwa taji zenye utukufu kupita zile taji walizovishwa viongozi wa mataifa ya dunia. Mfalme wa utukufu atakuwa amefuta machozi kwenye nyuso zote. Wataimba wimbo wa sifa ulio mtamu na wenye mpangilio mzuri. Wimbo utaongezeka na kujaza makao ya mbinguni. “Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Kisha wote wataitikia, “Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.” Ufunuo 7:10,12.TK 389.1

    Katika maisha haya tunaweza tu kuanza kuelewa mada kuu ya wokovu. Kwa uelewa wetu ulio na ukomo tunaweza kutafakari kwa umakini kuhusu aibu na utukufu, maisha na kifo, haki na rehema vilivyokutana msalabani; na bado hata kwa kutumia nguvu zetu zote za kiakili tunashindwa kuelewa umuhimu wake kikamilifu. Urefu na upana, kina na kimo cha upendo wa ukombozi vinaeleweka kidogo sana. Mpango wa ukombozi hautaeleweka kwa ukamilifu, hadi pale wale waliokombolewa watakapoona mambo jinsi yalivyo, na kuyajua mambo jinsi yanavyojulikana; lakini katika zama za milele ukweli mpya utaendelea kufunuliwa kwenye mioyo ya wale watakaokuwa wakishangaa kufurahi. Japo maumivu na uchungu na majaribu ya dunia yatakuwa yamekwisha na chimbuko lake kuondolewa, watu wa Mungu daima watakuwa na maarifa ya ufahamu wa pekee kukumbuka kile ukombozi wao ulichogharimu.TK 389.2

    Msalaba utakuwa wimbo wa waliokombolewa milele zote. Katika Kristo aliyetukuzwa watamwona Kristo aliYesulubishwa. Kamwe haitasahaulika kuwa Mwenye enzi wa mbinguni alijishusha ili amwinue mwanadamu aliyeanguka, kwamba aliibeba hatia na aibu ya dhambi na kufichwa kwa uso wa Baba yake hadi taabu za dunia iliyokuwa imepotea zilipouvunja moyo wake na kuyaangamiza maisha yake. Muumbaji wa ulimwengu wote aliuweka pembeni utukufu wake kwa sababu alimpenda mwanadamu-jambo hili daima litachochea mshangao wa ulimwengu wote. Mataifa ya waliokombolewa watakapomtazama Mwokozi na kutambua kwamba ufalme wake hauna mwisho, wataanza kuimba “Anastahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa na ametukomboa kutuleta kwa Mungu kwa damu yake ya thamani!”TK 389.3

    Mwujiza wa msalaba utaielezea miujiza yote. Itadhihirika kwamba yeye aliye na hekima isiyo na ukomo hangepanga mpango mwingine wa kutukomboa isipokuwa kafara ya Mwana wake. Fidia kwa ajili ya kafara itakuwa ni furaha ya kuijaza dunia na viumbe waliokombolewa, watakatifu, wenye furaha, na wasioweza kupatwa na mauti. Hiyo ndiyo thamani ya nafsi ambayo Baba anaridhishwa iliyolipwa. Na Kristo mwenyewe, atakapoyatazama matunda ya kafara yake kuu, ataridhika.TK 390.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents