Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jerome Apata Toba na Ujasiri Mpya

    Mara baada ya hapo aliletwa tena mbele ya baraza. Kujisalimisha kwake hakukuwaridhisha waamuzi. Ni kwa kuikana imani kikamilifu peke yake ambako kungeokoa uhai wake. Lakini alikuwa ameazimu kuitetea imani yake na kumfuata hadi kwenye moto ndugu yake aliyeifia dini.TK 72.2

    Aliikataa ile kauli yake ya kwanza ya kuacha mafundisho na, kama mtu anayekufa, alihitaji kwa heshima nafasi ya kuwasilisha utetezi wake. Maaskofu walisisitiza kwamba ilimpasa tu akubali au akatae madai yaliyoletwa dhidi yake. Jerome alipinga dhuluma hiyo ya kikatili. “Mmenifungia siku mia tatu na arobaini ndani ya gereza la kutisha,” alisema; “kisha mnanileta hapa mbele zenu, tena mkisikiliza adui zangu walio wanadamu tu, mnakataa kunisikiliza...Angalieni msitende dhambi dhidi ya haki. Mimi nilivyo, ni mwanadamu dhaifu; uhai wangu hauna umuhimu sana; na ninapowasihi msitoe hukumu isivyo haki, ninazungumza zaidi kuhusu ninyi kuliko mimi.” 28Ibid., pp 146, 147.TK 72.3

    Hatimaye, ombi lake lilikubaliwa. Mbele ya waamuzi wake, Jerome alipiga magoti na kuomba ili Roho wa Mungu atawale mawazo yake, ili kile alichotakiwa kunena kisiwe kinyume na ukweli kwa namna yoyote au kisichofaa kwa Bwana wake. Kwake yeye, ahadi hii ilitimia siku ile,TK 72.4

    “Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.” Mt. 10:19,20.TK 73.1

    Kwa mwaka mzima Jerome alikuwa amekaa ndani ya gereza lililo ardhini asiweze kusoma wala kuona. Licha ya hivyo, hoja zake ziliwasilishwa kwa uwazi na kwa nguvu kana kwamba alikuwa na nafasi ya kujifunza bila usumbufu. Aliwaelekeza wasikilizaji wake kwa orodha ndefu ya watakatifu waliohukumiwa na waamuzi ambao hawakufuata haki. Karibu kila kizazi wale waliotafuta namna ya kuwainua watu wa wakati wao walitupiliwa nje. Kristo mwenyewe alihukumiwa kama mhalifu kwenye mahakama ambayo haikuwa na haki.TK 73.2

    Sasa Jerome alitangaza toba yake na kushuhudia juu ya kutokuwa na hatia na utakatifu wa mfia dini Huss. “Nilimjua tangu utoto wake,” alisema. “Alikuwa mtu mzuri sana, mwenye haki na mtakatifu; alihukumiwa, bila kujali kutokuwa na hatia kwake...Nipo tayari kufa. Sitarudi nyuma ninapokuwa mbele ya mateso ambayo yameandaliwa na adui zangu na mashahidi wa uongo kwa ajili yangu, hawa ambao siku moja watawajibika kutoa taarifa ya ulaghai wao mbele za Mungu mkuu, ambaye hakuna awezaye kumdanganya.”TK 73.3

    Jerome aliendelea: “Katika dhambi zote ambazo nimewahi kutenda tangu ujana wangu, hakuna hata moja iliyo na uzito mkubwa mawazoni mwangu, na kunisababishia majuto makali, kama ile niliyotenda mahali hapa pa kufisha, wakati nilipokubali hukumu ile dhalimu iliyotolewa dhidi ya Wycliffe, na dhidi ya mfia dini mtakatifu, John Huss, bwana wangu na rafiki yangu. Ndiyo! Ninaikiri kutoka moyoni mwangu, na ninatamka nikiwa nimechukizwa kwamba nilinywea bila heshima, wakati ambapo kwa sababu ya hofu ya kifo, nilishutumu mafundisho yao. Kwa hiyo ninasihi... Mungu Mwenyezi akubali kusamehe dhambi zangu, na hususan hii, ambayo ni mbaya kuliko zote.”TK 73.4

    Akielekeza kwa waamuzi, alisema kwa uthabiti, “Uliwahukumu Wycliffe na John Huss...Mambo ambayo wameyasimamia, ambayo hayafai kupingwa, ninayafikiria na ninatamka, kuwa ninayapenda.” Maneno yake yalikatishwa. Maaskofu huku wakitetemeka kwa hasira, walipiga kelele: “Je, kuna hitaji gani la uthibitisho zaidi? Tunashuhudia hapa kwa macho yetu mzushi mwenye ukaidi kuliko wote!”TK 73.5

    Bila kutishwa na dhoruba, Jerome alisema kwa sauti: “Nini! Je, mnadhani ninaogopa kufa? Mmeniweka kwa mwaka mzima kwenye gereza la kutisha sana, zaidi ya mauti yenyewe.. .Siwezi kujizuia kueleza mshangao wangu kutokana na ukatili mkubwa kiasi hiki kwa Mkristo.” 29Bonnechose, vol. 2, pp. 151,153.TK 74.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents