Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukimya Mkubwa wa Agano Jipya

  Waprotestanti wanakiri kuwa kuna “ukimya mkubwa wa Agano Jipya kuhusu agizo la “Sabato” [Jumapili, yaani siku ya kwanza ya juma] au sheria zo zote kwa ajili ya kuiadhimisha.” 229.TK 278.3

  “Hadi wakati kifo cha Yesu, kulikuwa hakuna badiliko Io lote juu ya siku hiyo”; na “kulingana na kumbukumbu zilizoandikwa, mitume hawakuwahi ... kutoa agizo lo lote linalohusu kuiacha Sabato ya siku ya saba, na kuiadhimisha katika siku ya kwanza ya juma.” 230A. E. Waffle, The Lord’s Day , pp. 186-188.TK 278.4

  Wakatoliki wanakiri kwamba badiliko la Sabato lilifanywa na kanisa lao, na wanasema kwamba Waprotestanti, wanaitambua mamlaka ya Kanisa Katoliki kwa kuiadhimisha siku hiyo. Wanasema hivi: “Wakati wa sheria ya zamani, Jumamosi ilikuwa siku iliyotakaswa; lakini Kanisa, kwa kuagizwa na Yesu Kristu, na kuelekezwa na Roho wa Mungu, limeweka Jumapili badala ya Jumamosi; kwa hiyo sasa tunaitakasa siku ya kwanza, na siyo siku ya saba. Jumapili inamaanisha siku ya Bwana, na sasa ni siku ya Bwana.” 231Catholic Catechism of Christian Religion.TK 279.1

  Waandishi wa Kikatoliki hulielezea badiliko hilo kama ishara ya mamlaka ya Kanisa Katoliki, wakisema, “kitendo cha kuibadili Sabato kwenda Jumapili, jambo ambalo Waprotestanti wanaliafiki; ... kwani kwa kushika Jumapili, wanakiri uwezo wa Kanisa kuweka sikukuu, na kuamuru zishikwe chini ya dhambi.” 232Henry Tuberville, An Abridgement of the Christian Doctrine, p. 58.TK 279.2

  Sasa badiliko la Sabato ni nini? Kama siyo ishara au alama ya mamlaka ya Kanisa la Rumi—“alama ya mnyama?” Kanisa la Roma halijakanusha madai yake ya ukuu. Ulimwengu pamoja na makanisa ya Kiprotestanti wanapoafiki sabato iliyowekwa na kanisa hilo, huku wakiikataa Sabato ya Biblia, kimsingi wanakubaliana na madai hayo. Kwa kufanya hivyo wanaipuuza kanuni ambayo inawatofautisha na Kanisa la Roma— isemayo, “Biblia, Biblia pekee ndiyo dini ya Waprotestanti.” Kadiri harakati za kulazimisha ushikaji wa Jumapili zinavyozidi kukubalika, hatimaye zitauweka ulimwengu wote wa Kiprotestanti chini ya bendera ya Kanisa la Roma.TK 279.3

  Wakatoliki wanadai kuwa “uadhimishaji wa Jumapili kwa upande wa Waprotestanti ni heshima kubwa wanayoitoa, kwa mamlaka ya kanisa [Katoliki], kinyume cha msimamo wao wenyewe.” 233Mgr. Segur, Plain Talk About the Protestantism of Today, p. 213.TK 279.4

  Kulazimisha wajibu wa kidini kwa kutumia nguvu za dola kutaunda sanamu ya mnyama; hivyo kulazimisha ushikaji wa Jumapili nchini Marekani kutakuwa ni kulazimisha kumsujudia mnyama na sanamu yake.TK 279.5

  Wakristo wa vizazi vilivyopita walikuwa wanashika Jumapili wakidhani kuwa walikuwa wanashika Sabato ya Biblia, na hata sasa kuna Wakristo wa kweli katika kila kanisa wanaoamini kwa dhati kwamba Jumapili ni siku iliyochaguliwa na Mungu. Mungu anaukubali uaminifu na unyofu wao. Lakini ushikaji wa Jumapili utakapolazimishwa kisheria na ulimwengu utakapokuwa umepata nuru juu ya Sabato ya kweli, ye yote atakayeivunja amri ya Mungu na kutii sheria ya Kanisa la Roma, atakuwa ameiheshimu mamlaka ya Papa kuliko Mungu. Atakuwa anatoa heshima kwa Kanisa la Roma. Atakuwa anamsujudia mnyama na sanamu yake. Wakati huo watu watapokea alama ya utii kwa Kanisa la Roma—yaani “alama ya mnyama.” Haitakuwa hivyo mpaka suala hili liwekwe wazi mbele ya watu na wafike mahali pa kuchagua kati ya amri za Mungu na amri za wanadamu, ndipo wale wanaoendelea katika uasi watapokea “alama ya mnyama.”TK 280.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents