Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ufufuo wa Kwanza

    Wale “wahesabiwao kuwa wamestahili” ufufuo wa uzima wana “Heri, na mtakatifu” “...juu ya hao mauti ya pili haina nguvu” Luka 20:35; Ufunuo 20:6. Lakini wale ambao hawatapokea msamaha kupitia toba na imani “mshahara wa dhambi” adhabu “kwa kadiri ya matendo yao” wataishia katika “mauti ya pili”TK 333.3

    Kwa vile haitawezekana Mungu kumwokoa mwenye dhambi katika dhambi zake, atamnyang’anya uzima ambao uasi wake ulimwondoa kwa huo, atathibitika mwenyewe kuwa hakuustahili. “...bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.” “...nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.” Zaburi 37:10; Obadia 16. Wanazama bila tumaini na kusahauliwa milele.TK 333.4

    Hapo ndipo utakapofika mwisho wa dhambi. “Umemwaangamiza mdhalimu; Umelifuta jina lao milele na milele; Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele” Zaburi 9:5,6. Yohana, katika Ufunuo alisikia wimbo wa sifa wa watu wote ambao mpangilio wa sauti zake haujaharibiwa. Hakuna roho zilizopotea zitakazomkufuru Mungu zitakazokuwa zikitapatapa kwenye mateso yasiyokwisha. Hakuna viumbe wanyonge motoni ambao sauti za vilio vyao zitachangamana na nyimbo za waliookolewa.TK 333.5

    Juu ya uongo wa hali ya asili ya kutokufa kuna fundisho la hali ya kujitambua baada ya kufa. Kama ilivyo kwa somo la mateso ya milele, liko kinyume na Maandiko, ufahamu, na hisia zetu za ubinadamu.TK 334.1

    Kwa mujibu wa imani inayopendelewa na wengi, waliokombolewa walioko mbinguni wanajua kila kinachoendelea hapa duniani. Lakini inawezekanaje wafu wapate furaha wakijua taabu za walio hai, kuwaona wakivumilia huzuni, kuvunjika moyo, na maumivu makali ya maisha? Na inachukiza kiasi gani imani kwamba mara tu pumzi inapotoka katika mwili, roho ya yule aliyekufa inakwenda kwenye moto wa milele!TK 334.2

    Maandiko yanasemaje? Mtu akifa hana ufahamu: “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.” “walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno Io lote... Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.” “Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako. Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo” ~ ..mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?” Zaburi 146:4; Mhubiri 9:5, 6; lsaya 38:18, 19; Zaburi 6:5.TK 334.3

    Katika siku ya Pentekoste Petro alitamka kuwa Daudi “alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.” “Maana Daudi hakupanda mbinguni.” Ukweli kwamba Daudi atasalia kaburini hadi siku ya ufufuo unathibitisha kuwa wenye haki hawaendi mbinguni baada ya kifo.TK 334.4

    Paulo alisema: “Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.TK 334.5

    Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.” lWakorintho 15:16-18. Ikiwa kwa miaka 4,000 wenye haki walikwenda moja kwa moja mbinguni baada ya kifo, Paulo angewezaje kusema ikiwa hakuna ufufuo, “...wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.”?TK 334.6

    Alipokaribia kuwaacha wanafunzi wake, Yesu hakuwaambia kuwa bado kitambo wangeenda kwake: “...naenda kuwaandalia mahali.” Alisema. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu.” Yohana 14:2,3. Paulo anaongeza kutuambia, “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” Na anaongeza. “Basi, farijianeni kwa maneno hayo.”l Wathesalonike 4:16-18. Bwana atakapokuja pingu za kaburi zitavunjika na “waliokufa katika Kristo” watafufuliwa ili waishi milele.TK 334.7

    Watu wote watahukumiwa sawa sawa na mambo yaliyoandikwa katika vitabu na kupewa thawabu kama matendo yao yalivyokuwa. Hukumu hii haitafanyika siku ya kufa. “Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki” “Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote.” Matendo 17:31; Yuda 14,15.TK 335.1

    Lakini ikiwa wafu tayari wanafurahia mbinguni au wanateseka kwenye moto wa jahannamu, , hukumu ijayo ina kazi gani? Neno la Mungu linaweza kueleweka na watu wa kawaida. Lakini ni nini ambacho akili iliyo wazi itakiona, iwe hekima au haki katika nadharia iliyopo sasa? Je, wenye haki wataambiwa, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu,... ingia katika furaha ya Bwana wako,” baada ya kuishi mbele ya uso wake kwa muda mrefu? Je, waovu wataitwa watoke kwenye mateso ili waipokee hukumu kutoka kwa hakimu, “Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele”? Mathayo 25:21, 41.TK 335.2

    Nadharia ya hali ya kutokufa kwa roho ilikuwa moja ya mafundisho ya uongo ambayo Kanisa la Roma liliyaazima kutoka kwenye upagani. Luther aliliweka kundi moja na, “Kauli za uongo wa ajabu na wa kutisha ambazo zinaunda sehemu ya rundo la nyaraka za Mapapa wa Kanisa la Roma.” 234E. Petavel, The Problem of Immortality, p.255. Biblia inafundisha kwamba wafu wanalala hadi siku ya ufufuo.TK 335.3

    Pumziko lenye baraka kwa wenye haki waliochoka! Muda, hata kama utakuwa mrefu ama mfupi; ni kitambo tu kwao. Watalala; na wataamshwa kwa tarumbeta ya Mungu kwenye utukufu wa kutokufa. “...maana parapanda italia, na wafu watafufiiliwa, wasiwe na uharibifu,... Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.” 1 Wakorintho 15:52-54.TK 335.4

    Wataamshwa kutoka kwenye usingizi wao, wataanzia kufikiri pale walipoishia. Hisia za mwisho zilikuwa ni maumivu ya kifo; wazo la mwisho, kwamba walikuwa wanaangukia chini ya mamlaka ya mauti. Watakapoamka kutoka kaburini, wazo lao la kwanza la furaha litasikika katika kelele za ushindi: “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?” lWakorintho 15:55.TK 336.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents