Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Dhoruba Inakaribia

  Kadiri dhoruba inavyokaribia, kundi kubwa ambalo limeikiri imani katika ujumbe wa malaika wa tatu lakini hawajatakaswa kwa njia ya utii wa Maandiko wataziacha nafasi zao na kujiunga na upinzani. Kwa kuungana na dunia wamekuja kuyaona mambo karibia kwa uelewa ule ule, na wanachagua upande unaopendwa na wengi. Watu ambao hapo mwanzo walifurahia katika ukweli wanatumia talanta zao na hotuba nzuri kuzipotosha roho. Wanakuwa maadui wakali wa ndugu zao wa zamani. Waasi hawa ni mawakala madhubuti wa Shetani katika kuwawakilisha vibaya na kuwashtaki washika Sabato na kuwafanya watawala wawachukie.TK 367.1

  Watumishi wa Bwana wametoa onyo. Roho wa Bwana amewabidisha. . Hawajaangalia faida zao za kitambo au kufikiria kutunza heshima zao au maisha yao. Kazi inaonekana kubwa kuzidi uwezo wao wa kuikamilisha. Lakini pamoja na hayo hawawezi kurudi nyuma. Wakijisikia wasio kuwa na uwezo wa kufanya chochote, wanamkimbilia mwenye nguvu ili kupewa nguvu.TK 367.2

  Vipindi tofauti katika historia vimetambulika kwa maendeleo ya ukweli fulani wa pekee, ulipokelewa ili kukidhi mahitaji ya watu wa Mungu kwa wakati huo. Kila ukweli mpya umefaulu kuushinda upinzani. Mabalozi Wakristo lazima watekeleze majukumu yao na wamwachie Mungu matokeo.TK 367.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents