Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushindi kwa Wanamatengenezo

  Hizo ndizo njia Kanisa la Roma lilizitumia ili kuzima nuru ya Matengenezo na kurejesha ujinga na imani za kishirikina za Zama za Giza. Chini ya baraka za Mungu na utendaji kazi wa watu waadilifu aliowainua kuwa warithi wa Luther, Uprotestanti haukuangushwa. Haukupaswa kupata nguvu kutoka katika mikono ya wakuu. Mataifa madogo na dhaifu kabisa yaligeuka kuwa ngome imara. Ilikuwa ni mji mdogo wa Geneva; ilikuwa ni Uholanzi iliyokuwa inapigana na utawala wa kimabavu wa Hispania, nchi ya Sweden iliyo na baridi kali na isiyo na chochote, ndizo zilizoshinda kwa ajili ya Matengenezo.TK 152.1

  Kwa karibu miaka thelathini, Calvin alikuwa akitenda kazi pale Geneva ili kuendeleza Matengenezo katika Ulaya yote. Si kwamba mwelekeo wake haukuwa na dosari ama mafundisho yake hayakuwa na makosa. Lakini alikuwa ni msaada katika kuusambaza ukweli uliokuwa na umuhimu wa pekee, kufanya Uprotestanti uendelee kuwepo kukabiliana na mawimbi ya kasi ya kurejea kwa utawala wa Papa, na kukuza usafi na usahili katika maisha.TK 152.2

  Kutokea Geneva, machapisho na walimu walikwenda kusambaza mafundisho ya matengenezo. Kutoka hapa waliokuwa wanateswa kwenye nchi zote walipata maelekezo na kutiwa moyo. Mji wa Calvin ulikuwa kimbilio la usalama kwa Wanamatengenezo wote waliokuwa wanawindwa kwenye eneo lote la Ulaya ya Magharibi. Walikuwa wanakaribishwa na kuhudumiwa vizuri, walipopata makazi hapa waliubariki mji ulio wa asili kwa ujuzi, elimu, na kwa kicho chao kwa Mungu. Mwanamatengenezo shujaa wa Scotland aliyekuwa anaitwa John Knox, Waprotestanti wengi walioitwa Puritans wa Uingereza, Waprotestanti wa Uholanzi na Hispania, na Waprotestanti wa Ufaransa waliokuwa wanaitwa Hugenots, waliuchukua mwenge wa ukweli kutoka Geneva na kwenda kuuangaza kwenye giza lililokuwa kwenye nchi walizokuwa wamezaliwa.TK 152.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents