Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuzifuta Dhambi

  Kazi ya hukumu ya upepelezi na kuzifuta dhambi itakamilika kabla ya kuja kwa Bwana mara ya pili. Katika zile huduma kielelezo(patakatifu pa duniani), kuhani mkuu alikuwa anatoka nje ya hema ya kukutania na kulibariki kusanyiko. Vivyo hivyo Kristo, atakaRomaliza kazi yake kama mpatanishi, atatokea, “Pasipo dhambi, kwa wokovu.” Waebrania 9:28.TK 300.3

  Kuhani mkuu alipokuwa anaziondoa dhambi kutoka kwenye hema ya kukutania, aliziungama akiweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa Azazeli. Kristo ataziweka dhambi hizi zote juu ya Shetani, ambaye ni mwanzilishi wa dhambi. Mbuzi wa Azazeli alipelekwa mbali “mpaka nchi isiyo watu.” Mambo ya Walawi 16:22. Shetani, atafungwa kwa miaka elfu moja kwenye dunia iliyo ukiwa, akiwa amebeba hatia ya dhambi alizowashawishi watu kutenda, na mwishowe atateseka kwa adhabu ya moto utakaowateketeza waovu. Hivyo mpango wa wokovu utafikia utimilifu wake wakati dhambi itakapong’olewa.TK 300.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents