Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 34 - Roho Nl Nani Katika Imani Ya Mizimu?

    Fundisho la hali ya asili ya kutokufa,-awali liliazimwa kutoka kwenye falsafa ya wapagani na wakati wa giza kuu la uasi lilijumuishwa kwenye imani ya Ukristo, sasa limechukua nafasi ya ukweli kwamba, “...wafu hawajui neno lolote”. Mhubiri 9:5. Watu wengi wanaamini kuwa roho za wafu ndizo, “...roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” Waebrania 1:4.TK 337.1

    Imani kwamba roho za wafu zinarudi kuwahudumia waliohai imefungua mlango kwa ajili ya imani ya kisasa ya mizimu. Ikiwa wafu wanapata fursa ya kuwa na maarifa yanayozidi yale waliyokuwa nayo wakiwa hai, kwa nini wasirudi duniani ili wawafundishe walio hai? Ikiwa roho za wafu huvinjari juu ya rafiki zao duniani, kwa nini zisiwasiliane nao? Ni kwa namna gani wale wanaoamini kuwa mwanadamu anajitambua baada ya kifo wanaikataa “nuru ya Mungu” iliyoletwa na roho wenye utukufu? Hii ni njia inayotiliwa maanani kuwa ni takatifu ambayo kwayo Shetani anafanya kazi. Malaika walioanguka wanaonekana kama wajumbe kutoka katika ulimwengu wa roho.TK 337.2

    Mkuu wa uovu anao uwezo wa kuleta mbele ya wanadamu mwonekano wa rafiki zao waliokufa. Sura ya bandia itaonekana ni kamilifu, imetengenezwa kwa ubainifu wa ajabu. Wengi wanafarijika kwa uhakika kwamba wapendwa wao waliokufa wana fursa ya kuwa mbinguni. Pasipo hisia za hatari wanasikiliza, “roho zidanganyazo” lTimotheo 4:1TK 337.3

    Wale waliokufa pasipo matayarisho wanadai kuwa wana furaha na wanashika nyadhifa za juu mbinguni. Hawa wageni wakujifanya kutoka kwenye ulimwengu wa roho wakati mwingine wanatoa maonyo ambayo yanathibitika kuwa ni sahihi. Kisha, kwa sababu wameaminika, wanaleta mafundisho yanayoshusha hadhi ya Maandiko. Ukweli kwamba wanatoa baadhi ya kauli za kweli na pengine kubashiri matukio ya siku za usoni unawafanya kuaminika, na mafundisho yao potovu kukubalika. Sheria ya Mungu imewekwa kando, Roho wa neema amedhihakiwa. Hizo roho zinaukataa Uungu Wakristo na kumweka Mwumbaji daraja moja na wao. Wakati ni ukweli kwamba matokeo ya hila yamekuwa na ushawishi kana kwamba ni udhihirisho wa kweli, kumekuwa na maonesho wazi ya nguvu za miujiza, ambazo ni kazi za moja kwa moja za Shetani. Wengi wanaamini kuwa imani ya mizimu ni ulaghai tu wa wanadamu. Watakapokutana uso kwa uso na udhihirisho ambao watauona kama miujiza, watadanganyika na kuukubali kuwa ni uwezo mkuu ya Mungu.TK 337.4

    Kwa msaada wa kishetani wachawi wa Farao waliiga kazi ya Mungu kwa udanganyifu. Angalia Kutoka 7:10-12. Paulo anashuhudia kuwa kuja kwa Bwana kutatanguliwa na “kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea” 2Wathesalonike 2:9,10. Na Yohana anatamka kuwa: “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya” Ufunuo 13:13,14. Hapa si ulaghai tu wa wanadamu uliotabiriwa. Wanadamu wanadanganyika kwa miujiza ambayo mawakala wa Shetani wanatenda, na siyo ile wanayojifanya kuitenda.TK 338.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents