Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mabishano Na Watawala wa Kanisa la Roma

    Kwa kuona mafanikio kidogo yaliyopatikana kwa mateso ya kujaribu kukandamiza kazi ya Luther nchini Ujerumani, Watawala wa Kanisa la Roma waliamua kufanya mashindano ya maneno na Zwingli.Wangejihakikishia ushindi si tu kwa kuchagua sehemu ya kufanyia bali pia waamuzi na watu watakaoshiriki katika pambano hilo. Na ikiwa wangemtia Zwingli mikononi mwao, wangemlinda sana asije akawatoroka. Hata hivyo kusudi hili lilifanywa kwa kificho na uangalifu mkubwa.TK 117.3

    Mabishano yalipangwa kufanyika kule Baden. Kwa kushuku makusudio ya watawala wa kanisa la Papa na likiwa limetahadharishwa na moto ulikuwa ukiwashwa kuwateketeza watu waliokuwa wakiikiri Injili kwenye majimbo yaliyokuwa chini yao; Baraza la Zurich lilimkataza mchungaji wao kujiingiza katika hatari hiyo. Kwenda Baden mahali ambapo damu ya wafiadini kwa ajili ya ukweli ilimwagwa, ilikuwa hakika ni kukiendea kifo. Waliochaguliwa kuwawakilisha Wanamatengenezo walikuwa ni Oecolampadius na Haller; wakati Dk. Eck akisaidiwa na kundi la madaktari wasomi na maaskofu, ndiye aliyekuwa mtetezi wa Kanisa la Roma.TK 118.1

    Makarani wote walikuwa wamechaguliwa na watawala wa kanisa la Papa, na watu wengine hawakuruhusiwa kuandika chochote, vinginevyo wangekabiliwa na kifo. Hata hivyo mwanafunzi fulani aliyekuwa akihudhuria kwenye mipango hiyo aliandika kila kilichokuwa kinajadiliwa kila siku. Karatasi hizi zilichukuliwa na wanafunzi na kupelekwa pamoja na barua zilizopelekwa kwa Oecolampadius na Zwingli kila siku kule Zurich. Mwanamatengenezo huyo alijibu na kutoa ushauri. Ili kuepuka macho ya walinzi wa malango ya mji, wajumbe hawa walikuja na vikapu vya kuku vichwani mwao na waliruhusiwa kupita bila kipingamizi.TK 118.2

    Myconius alisema, “Zwingli amefanya kazi sana kuliko ambavyo angefanya kwa kujadiliana na mtu ana kwa ana katikati ya maadui zake, kwa tafakari zake, akipitisha nyakati za usiku bila kulala, na ushauri ule aliokuwa anaupeleka Baden.” 104D’Aubigne, bk. 11, ch. 13.TK 118.3

    Wawakilishi wa Kanisa la Roma walikuja Baden wakiwa wamevalia mavazi yao ya fahari na vito vilivyokuwa vinang’aa. Walisafm kianasa, meza zao zilijaa vyakula vya gharama kubwa na mvinyo waliokuwa wakinywa ulikuwa wa viwango vya juu kabisa. Kulionekana tofauti kubwa kati yao na Wanamatengenezo ambao walikuwa wakitumia walivyokuwa navyo kwa uangalifu huku wakitumia muda mfupi katika meza ya chakula. Mwenye nyumba aliyokuwa anakaa Oecolampadius alitumia muda wake kufuatilia alichokuwa anafanya mpangaji wake na kugundua kuwa, mara nyingi alimkuta anasoma au anaomba, na kutoa taarifa ya kwamba alikuwa kwa kiasi fulani “Mcha Mungu sana.”TK 118.4

    Kwenye mkutano ule, “Eck alisimama kwenye mimbari kwa majivuno makubwa akiwa amevalia mavazi ya fahari yaliyopambwa; wakati Oecolampadius aliyeonekana mnyenyekevu, aliyekuwa amevaa mavazi ya kawaida, alilazimishwa kuketi mbele ya mpinzani wake kwenye kiti kilichokuwa kimetengenezwa vibaya.” Sauti kubwa na yenye kuunguruma ya Eck na moyo wa kujiamini aliokuwa nao havikumbabaisha. Yule ambaye angeitetea imani yake angepewa donge nono. Wakati alipotindikiwa na hoja za maana, Eck aligeukia matusi na kulaani.TK 119.1

    Mwonekano wa Oecolampadius usioonesha majivuno na kujitumainia nafsi ulikuwa umenywea kwenye mabishano hayo. Japokuwa alionekana mpole na mwenye heshima, alithibitisha uwezo wake bila wasiwasi wala woga wowote. Kwa uthabiti, Mwanamatengenezo huyu aling’ang’ania kwenye Maandiko. Alisema, “Desturi hazina nguvu katika Uswisi yetu, vinginevyo ziwepo kwa mujibu wa katiba; na katika masuala ya imani, Biblia ndiyo katiba yetu.” 105Ibid.TK 119.2

    Utulivu aliokuwa nao Mwanamatengenezo huyu na jinsi alivyotoa hoja kwa ufasaha, alivyozitoa kwa upole na bila majivuno, aliwagusa watu kiasi cha kuyaona maneno ya Eck yasiyohakikishwa na yaliyokuwa yametolewa kwa majivuno kuwa karaha tupu.TK 119.3

    Kwa siku kumi na nane mjadala uliendelea. Wawakilishi wa kanisa la Papa walidai kuwa walikuwa wameshinda. Wengi wa wabunge walisimama upande wa Kanisa la Roma, na baraza lote lilitamka ya kwamba Wanamatengenezo walikuwa wameshindwa vibaya na kutangaza ya kuwa wao pamoja na Zwingli walikuwa wametengwa kutoka katika kanisa. Hata hivyo majadiliano hayo yalisababisha mchocheo thabiti kwa Uprotestanti. Muda mfupi baadaye miji muhimu ya Bem na Basel ilitangaza kujiunga kwenye Matengenezo.TK 119.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents