Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    “Haya, Bwana Arusi”

    Kuja kwa Kristo kwenye patakatifu sana kama Kuhani Mkuu kwa ajili ya kupatakasa patakatifu (Dan. 8:14), kuja kwa aliye mfano wa mwanadamu kwa Mzee wa Siku (Danieli 7:13), na kuja kwa Bwana katika hekalu lake (Malaki 3:11) ni tukio moja. Jambo hili linawakilishwa pia na kuja kwa bwana arusi kwenye arusi katika mfano wa wanawali kumi wa Mathayo 25.TK 266.2

    Katika mfano huo, bwana arusi alipokuja, “wale waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.” Kuja huku kwa bwana arusi kulitokea kabla ya arusi. Arusi inawakilisha Kristo kupokea ufalme wake. Mji Mtakatifu, Yerusalemu Mpya, mji mkuu na kiwakilishi cha huo ufalme, unaitwa, “bibi arusi, mke wa Mwanakondoo.” Malaika alimwambia Yohana: “Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.” “Akanichukua katika Roho”, nabii Yohana anasema, “akanionyesha ule mji mtakatifii, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.” Ufunuo 21:9, 10.TK 266.3

    Bibi arusi anawakilisha ule Mji Mtakatifu, na wale wanawali waliokwenda kumlaki bwana arusi ni kielelezo cha kanisa. Katika Ufunuo watu wa Mungu wanaonekana kuwa wageni katika karamu ya arusi. Kama ni wageni, basi hawawezi kuwa bibi arusi. Kristo atapokea kutoka kwa Mzee wa Siku “mamlaka, na utukufu, na ufalme,” Yerusalemu mpya, makao makuu ya ufalme wake, ulioandaliwa, “kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.” Baada ya kuupokea ufalme, atakuja kama Mfalme wa Wafalme na Bwana wa mabwana kwa ajili ya ukombozi wa watu wake ambao watashiriki katika karamu ya arusi ya Mwana-kondoo. Danieli 7:14; Ufunuo 21:2.TK 267.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents