Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kazi ya Mwisho ya Patakatifu

    Katika mfano wa Mathayo 22, hukumu ilifanyika kabla ya arusi. Kabla ya arusi mfalme alikuja kuona kama wageni wote wamevaa vazi la arusi, vazi lisilo na mawaa la tabia iliyooshwa katika damu ya Mwana Kondoo. Ufunuo 7:14. Wote walioonekana na vazi la arusi baada ya ukaguzi walikubaliwa na kuhesabiwa kuwa walikuwa wanastahili kushiriki katikaTK 267.4

    ufalme wa Mungu na kuwa na sehemu katika kiti chake cha enzi. Kazi hii ya uchunguzi wa tabia ni hukumu ya upelelezi, kazi ya mwisho ya patakatifu pa mbinguni.TK 268.1

    Mashauri ya wale ambao wamekuwa wakimkiri Yesu katika enzi zote yatakapokuwa yameamuliwa, muda wa matazamio utakwisha na mlango wa rehema utafungwa. Hivyo kwa sentensi moja fupi isemayo “Nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa,” tunapelekwa katika wakati ambapo kazi kubwa ya wokovu wa mwanadamu itakamilika.TK 268.2

    Wakati kuhani mkuu alipokuwa anaingia patakatifu sana siku ya upatanisho, huduma katika chumba cha kwanza ilikuwa inasimama. Kwa hiyo Kristo alipoingia patakatifu sana kufanya kazi ya mwisho ya upatanisho, alikomesha huduma yake katika hema ya kwanza. Wakati huo huduma katika chumba cha pili ilianza. Kristo alikuwa amekamilisha sehemu moja tu ya kazi yake kama mwombezi, na kuingia katika sehemu nyingine ya kazi hiyo. Bado alikuwa anasihi mbele ya Baba kwa kwa niaba ya wenye dhambi kwa kutumia damu yake.TK 268.3

    Wakati ni kweli kwamba mlango wa matumaini na rehema ambao wanadamu walipitia kwenda kwa Mungu kwa miaka 1800 ulikuwa umefungwa, mlango mwingine ulifunguliwa. Msamaha wa dhambi ulikuwa unatolewa kuwa njia ya uombezi Wakristo akiwa patakatifu sana. Bado kulikuwa na mlango “ulio wazi” wa kuingia patakatifu, ambapo Kristo alikuwa anahudumu kwa niaba ya mwenye dhambi Sasa palioenekana mahali pa kuyatumia maneno ya Kristo aliyoyasema katika Ufunuo, ambayo yalikuwa yemelenga wakati huu hasa: “Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye ... Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga.” Ufunuo 3:7, 8.TK 268.4

    Wale wanaomfuata Yesu katika kazi kubwa ya upatanisho hunufaika na uombezi wake, wakati wale wanaoikataa nuru hiyo hawanufaiki nayo. Wayahudi ambao walikataa kumwamini Yesu kama Mwokozi hawakuweza kupata msamaha kupitia kwake. Yesu alipoingia patakatifu pa mbinguni baada ya kupaa kwake na kuwamwagia wanafunzi wake baraka za uombezi wake, Wayahudi waliachwa katika giza nene wakiendelea kutoa dhabihu na sadaka sisizo na maana. Mlango ambao mwanzoni watu walikuwa wanaingilia ulikuwa hauko wazi tena. Wayahudi walikuwa wamekataa kumtafuta katika njia pekee aliyokuwa anaweza kupatikana, yaani kwa njia ya patakatifu pa mbinguni.TK 268.5

    Wayahudi ambao hawakuamini, ni kilelezo cha wale wasiojali na wasioamini miongoni mwa wale wanaojiita Wakristo ambao hawaielewi kazi ya Kuhani wetu Mkuu kwa kujitakia wenyewe. Katika ile huduma ya kilelezo, kuhani mkuu alipokuwa anaingia patakatifu sana, Israeli wote walikuwa wanatakiwa kukusanyika kupazunguka patakatifu na kunyenyekeza nafsi zao mbele za Mungu, ili wapate msamaha wa dhambi na ili wasikatiliwe mbali na kusanyiko. Ni muhimu zaidi katika siku hii halisi ya upatanisho, tuielewe kazi ya Kuhani wetu Mkuu na kuyajua majukumu anayotaka tuyatimize.TK 269.1

    Katika siku za Nuhu, ujumbe ulitumwa kutoka mbinguni, na wokovu wao ulikuwa unategemea jinsi walivyouchukulia ujumbe huo. Mwanzo 6:6-9; Waebrania 11:7. Wakati wa Sodoma, watu wote waliteketezwa na moto uliokuwa umetoka mbinguni isipokuwa Lutu na binti zake wawili. Mwanzo 19. Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Kristo. Mwana wa Mungu aliwaambia Wayahudi wasioamini: “Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.” Mathayo 23:38. Ukizitazama siku za mwisho, uwezo huo huo usio na kikomo unasema juu ya wale ambao “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo.” 2 Wathesalonike 2:10, 11. Wanapoyakataa mafundisho ya Neno lake, Mungu humwondoa Roho wake na kuwaacha katika udanganyifu ambao wanaupenda. Lakini Kristo bado anaomba kwa ajili ya mwanadamu, na nuru itatolewa kwa wale wanaoitafuta.TK 269.2

    Kupita kwa wakati mwaka 1844 kulifuatiwa na jaribu kubwa kwa wale waliokuwa na imani ya Ujio. Nafuu yao pekee ilikuwa ile nuru iliyoelekeza akili zao katika patakatifu pa mbinguni. Walipokuwa wanangoja na kuomba, waliona kwamba Kuhani wao Mkuu alikuwa ameingia katika kazi nyingine ya huduma. Wakimfuata kwa imani, walioneshwa pia kazi ya mwisho ya kanisa. Waliuelewa zaidi ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili, na walikuwa tayari kupokea na kutoa onyo nyeti la malaika wa tatu wa Ufunuo 14 kwa ulimwengu.TK 269.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents