Kuungana na Ulimwengu
Makanisa mengi ya Kiprotestanti yamefuata nyayo za Kanisa la Roma kwa kushikamana na “wafalme wa dunia”—yaani, makanisa ya kitaifa, kwa kushikamana na serikali za kidunia; na madhehebu mengine, kwa kutaka kupendwa na ulimwenguni. Neno “Babeli” (au, machafuko) linaweza kuwakilisha taasisi hizi zinazodai kuwa zinatoa mafundisho katika Biblia, lakini zimegawanyika katika madhehebu nyingi zenye mafundisho yanayopingana.TK 243.2
Kitabu kimoja cha Kikatoliki kinasema kwamba “kama Kanisa la Roma lina hatia ya ibada ya sanamu kwa sababu ya watakatifu; binti yake Kanisa la Uingereza, ana hatia hiyo hiyo kwani ana makanisa kumi yaliyopewa heshima ya Mariamu kwa kila kanisa moja lililopewa heshima ya Kristo.” TK 243.3
Naye Dk. Hopkins anasema: “Hakuna sababu ya kudhania kuwa tabia na desturi za upinga Kristo zinahusu kanisa ambalo leo linaitwa Kanisa la Roma. Makanisa ya Kiprotestanti yana upinga Kristo mwingi, na bado hayajabadilika ipasavyo ... kutoka katika ufisadi na uovu.” TK 243.4
Kuhusu Kanisa la Presbyterian kujitenga na Kanisa la Roma, Dk. Guthrie aliandika: “Miaka mia tatu iliyopita, kanisa letu, likiwa na Biblia iliyo wazi katika nembo yake, na mwito usemao “Yachunguzeni Maandiko” katika bango lake, lilitoka katika malango ya Roma.” Kisha aliuliza swali muhimu: “Je walitoka Babeli wakiwa safi?” TK 243.5