Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Zahama ya Kutisha

    Hiyo ilikuwa ni Zahama ya kutisha kwa Matengenezo. Luther hakuwa kipofu kwa ajili ya dhoruba iliyokuwa karibu kufumuka, lakini alimtumaini Kristo awe msaada na ngao yake. “Kile kinachokaribia kutokea sikijui, na wala sijishughulishi kukijua...Jani halitaanguka bila mapenzi ya Baba. Ni kwa kiasi gani basi anatujali sisi! Ni kitu rahisi kufa kwa ajili ya Neno, maana Neno aliyefanyika mwili Yeye mwenyewe alikufa” 60D’Aubigne, 3’1 London ed., Walther, 1840, bk. 6, ch. 9.TK 91.5

    Amri ya Papa ilipomfikia Luther, alisema, “Ninaidharau na kuishambulia, kuwa ina kufuru, ni ya uongo...Ni Kristo mwenyewe aliyeshutumiwa ndani yake. Tayari ninahisi uhuru mkubwa moyoni mwangu; maana hatimaye ninafahamu kwamba Papa ni mpinga Kristo, na kwamba kiti chake ni kile cha Shetani mwenyewe.” 61Ibid.TK 92.1

    Siyo kwamba mamlaka ya Kanisa la Roma ilikuwa bure. Watu dhaifu na waliokuwa wanashika mapokeo potovu, walitetemeka kwa ajili ya amri ya Papa, na wengi walihisi kuwa uhai ni bora sana na haungepaswa kuhatarishwa. Je, kazi ya Mwanamatengenezo ilikaribia kufungwa?TK 92.2

    Luther bado hakuogopa. Kwa nguvu ya ajabu aliitupilia mbali hukumu Kanisa la Roma. Mbele ya umati mkubwa wa raia wa ngazi zote, Luther aliichoma moto amri ya Papa. Alisema, “Pambano zito ndiyo limeanza. Kabla ya hapo nilikuwa tu nacheza na Papa. Niliianza kazi hii kwa jina la Mungu; na itamalizika bila mimi, na kwa nguvu zake...Ni nani ajuaye kwamba Mungu hajanichagua na kuniita mimi, na kama hawapaswi kuliogopa hilo, kwa kunidharau mimi, wanamdharau Mungu mwenyewe?...TK 92.3

    Mungu hajawahi kumchagua kuhani mkuu au mtu mwenye cheo kikubwa kuwa nabii; bali huwachagua watu duni na wanaodharauliwa, mara moja alimchagua Amosi mchungaji. Katika kila kizazi, watakatifu waliwakemea wakuu, wafalme, wana wa wafalme, makuhani, na watu wenye hekima, wakihatarisha maisha yao... Sisemi kuwa mimi ni nabii; bali nasema kuwa inawapasa kuwa na hofu kidogo kwa sababu niko pekee yangu na wao wako wengi. Nina uhakika na hili, kwamba Neno la Mungu liko upande wangu, na kwamba haliko kwao.” 62Ibid.,ch. 10.TK 92.4

    Uamuzi wa mwisho wa Luther kujitenga na kanisa uliambatana na pambano la kutisha ndani ya nafsi yake: “Oo ni maumivu kiasi gani yaliyonipata, ingawa nilikuwa na Maandiko upande wangu, kuhalalisha mwenyewe kwamba inanipasa kuthubutu kuwa na msimamo wa peke yangu dhidi ya Papa, na kumtaja kuwa ni mpinga Kristo! Ni mara ngapi sikujiuliza kwa uchungu lile swali, ambalo mara nyingi sana, lilikuwa midomoni mwa watawala wa Kanisa la Roma kwamba: ‘Je, peke yako u mwenye hekima? Je, inawezekana kuwa kila mmoja amekosea? Itakuwaje, ikiwa baada ya yote, itaonekana kuwa ni wewe mwenye makosa na unawahusisha wengi katika makosa, ambao hatimaye watapotea milele?’ Ndivyo nilivyopigana mwenyewe pamoja na Shetani, hadi Kristo, kwa njia ya Neno lake lisilokosea, alipouimarisha moyo wangu dhidi ya mashaka haya.” 63Martyn, pp. 372, 373.TK 93.1

    Amri mpya ikatolewa, ikitangaza hatua ya mwisho ya kutengwa kwa Mwanamatengenezo kutoka kwenye Kanisa la Roma, likimshutumu kuwa amelaaniwa mbinguni, na kwamba wote ambao wangeyapokea mafundisho yake wangehusika katika hukumu hiyo.TK 93.2

    Upinzani ni fungu la wote ambao Mungu huwatuma kuupeleka ukweli hasa ule unaofaa kwa wakati wao. Kulikuwa na ukweli wa leo katika siku za Luther; kuna ukweli wa leo kwa ajili ya kanisa leo. Lakini ukweli haupendwi sana na wengi leo kuliko ilivyokuwa kwa watawala wa kanisa la Papa, waliompinga Luther. Wale wanaouleta ukweli wa wakati huu haiwapasi kutarajia kuwa watapokelewa kwa upendeleo mkubwa kuliko ilivyokuwa kwa wanamatengenezo wa awali. Pambano kuu baina ya ukweli na uongo, baina ya Kristo na Shetani, litazidi wakati historia ya ulimwengu inapoelekea kufungwa. Angalia Yohana 15:19, 20; Luka 6:2.TK 93.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents