Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuinua Mamlaka Ya Binadamu

    Kristo alikuwa na mtazamo wa kiunabii kuhusu kazi ya kuinua mamlaka ya kibinadamu itakayotawala dhamiri, ambayo imekuwa laana mbaya katika zama zote. Maonyo yake kuhusu kutowafuata viongozi vipofu yamewekwa kwenye kumbukumbu kuwa tahadhari kwa vizazi vijavyo.TK 360.2

    Kanisa Katoliki linawapa viongozi wake haki ya kufasili Maandiko. Ijapokuwa matengenezo yaliruhusu Maandiko kwa watu wote, bado kanuni ile ile iliyotumiwa na Kanisa la Roma inawazuia watu wengi katika makanisa ya kiprotestanti kutojisomea Maandiko wao wenyewe. Wanafundishwa kuyapokea mafundisho yake kama yanavyofasiliwa na kanisa. Maelfu hawapati chochote, hawayafahamu Maandiko jambo ambalo ni kinyume na imani zao.TK 360.3

    Wengi wako tayari kusalimisha mioyo yao kwa wachungaji. Pasipo kujua wanayaacha mafundisho ya Mwokozi. Lakini je wachungaji hawawezi kukosea? Tunawezaje kuamini mwongozo wao isipokuwa tumejifunza kutoka katika Neno la Mungu ya kuwa wao ni wabeba nuru? Upungufu wa ujasiri wa kimaadili unawafanya wengi kuwafuata wasomi na wanaishia kwenye makosa pasipo matumaini. Wanauona ukweli wa wakati huu ndani ya Biblia na wanaona Roho Mtakatifu akiongoza ujumbe unaohubiriwa, lakini bado wanawaruhusu wachungaji kuwaondoa kutoka kwenye nuru.TK 360.4

    Shetani anawashikilia watu wengi kwa kuwaunganisha kwa kamba za urafiki na wale ambao ni maadui wa msalaba Wakristo. Muungano huu waweza kuwa wa wazazi, wa mtoto wa kike au kiume, wa ndoa au wa kijamii. Roho za watu katika hali ya kuhangaika hazina ujasiri wa kuyatii yale wanayoyaamini kuwa ni wajibu wao.TK 361.1

    Wengi watasema haidhuru kile mtu anachokiamini, ikiwa maisha yake ni sahihi. Lakini maisha hujengwa na imani. Kama ukweli uko ndani ya uwezo wetu kuufikia na tukashindwa kuuzingatia tutakuwa tumeukataa tukichagua giza badala ya nuru.TK 361.2

    Kutojua isiwe kisingizio cha kosa au dhambi, wakati kila fursa ipo ya kufahamu mapenzi ya Mungu. Mtu anayesafiri akifika sehemu ambapo kuna barabara kadhaa na kuna mabango yanayoonesha kila moja iendako, ikiwa atapuuzia yale mabango na kupita njia yoyote aonayo kuwa sahihi, anweza kufanya hivyo lakini atajikuta katika njia isiyo sahihi.TK 361.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents