Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kutokuwa Na Kiasi KumewapumbazaWengi

  Mahakama zimepotoka, watawala wanasukumwa na tamaa ya kulimbikiza mali na kupenda anasa. Kutokuwa na kiasi kumewapumbaza wengi kiasi kwamba Shetani amewatawala kabisa. Mahakimu wamepotoka, wanahongwa kwa rushwa na kudanganywa. Ulevi na fujo, kukosa uaminifu wa kila namna, kumeshamiri miongoni mwa wale wanaozisimamia sheria. Hivi sasa kwasababu Shetani hawezi tena kuudhibiti ulimwengu kwa kuyaficha Maandiko, anatumia njia nyingine kutimiza lengo hilo. Kuiharibu imani katika Biblia kunafanya kazi sawa na kuiharibu Biblia yenyewe.TK 354.4

  Kama ilivyokuwa kwa vizazi vilivyopita, Shetani ametenda kazi kupitia makanisa kuendeleza mipango yake. Katika kuushambulia ukweli usiopendwa, wanazikubali fasili ambazo zinatawanya mbegu za mashaka. Wakiyang’ang’nia makosa ya mamlaka ya Papa ya hali ya kutokufa kwa nafsi na hali ya mwanadamu kuwa na ufahamu baada ya kufa wanakataa kinga yao ya pekee dhidi ya imani ya mizimu. Fundisho la mateso ya milele limewafanya wengi kutoiamini Biblia. Kadiri madai ya amri ya nne yanavyosisitizwa, inaonekana kuwa ushikaji wa Sabato ya siku ya saba unatolewa agizo; na kama njia pekee kwao kujiweka huru kutoka kwenye wajibu ambao hawako radhi kuutekeleza, walimu wanaopendwa wanaitupa mbali sheria ya Mungu pamoja na Sabato. Kadiri matengenezo kuhusu Sabato yanavyoendelea, kukataliwa kwa sheria ya Mungu ili kuepuka amri ya nne kutaenea karibu ulimwengu mzima. Viongozi wa kidini wataruhusu ukafiri, imani ya mizimu na dharau kwa sheria takatifu ya Mungu-wajibu wa kutisha kwaajili ya uovu uliopo kwenye ulimwengu wa Kikristo.TK 355.1

  Na bado kundi hili hili la watu litadai kuwa ulazimishaji wa amri ya Jumapili utaboresha maadili ya jamii. Ni mojawapo ya hila za Shetani kuchanganya uongo na ukweli mwingi ili uonekane kuwa ni kitu cha kukubalika. Viongozi wa harakati za amri ya Jumapili wanaweza kutetea matengenezo ambayo watu wayanahitaji, kanuni zinazopatana na Biblia, lakini kwa kuwa pamoja na hayo kuna hitaji linalopingana na sheria ya Mungu, watumishi wake hawataungana nao. Hakuna kiwezacho kuhalalisha uwekaji kando wa sheria za Mungu kwa ajili ya kutimiza maagizo ya wanadamu.TK 355.2

  Kwa kutumia makosa mawili makubwa, hali ya kutokufa kwa roho na utakatifu wa Jumapili, Shetani atawaweka watu chini ya udanganyifu wake. Wakati kosa la kwanza linaweka msingi wa imani ya mizimu, lile la pili linatengeneza kiungo cha wema wa Kanisa la Roma. Waprotestanti wa Marekani watakuwa mstari wa mbele kunyosha mikono yao ili kuvuka shimo kubwa na kuushika mkono wa imani ya mizimu; watalivuka lindi kuu na kupeana mikono na mamlaka ya Kanisa la Roma; na chini ya ushawishi wa huu muungano wenye sehemu tatu mashirika matatu nchi hii (Marekani) itafuata nyayo za Kanisa la Roma katika kukanyaga haki za dhamiri.TK 355.3

  Imani ya mizimu inaponaigiza Ukristo wa wakati huu, inakuwa na uwezo mkubwa wa kudanganya. Ibilisi mwenyewe “ameongoka.” Atatokeza kama malaika wa nuru. Kwa njia ya imani ya mizimu, miujiza mingi itatendeka, wagonjwa wataponywa, na maajabu mengi yasiyoweza kupingika yatatendeka.TK 356.1

  Wafuasi wa Papa wanaojivunia miujiza kama ishara ya kanisa la kweli watadanganywa upesi na uwezo huu utendao miujiza, na Waprotestanti, wakiwa wameitupilia mbali ngao ya ukweli, watadanganywa pia. Wafuasi wa Papa, Waprotestanti, na watu wa dunia wote kwa pamoja wataona ndani ya harakati kuu kwa ajili ya kuuongoa ulimwengu.TK 356.2

  Kwa njia ya imani ya mizimu, Shetani anaonekana kuwa ndiye mfadhili wa jamii ya wanadamu, akiponya magonjwa na kuleta mfumo mpya wa imani ya kidini, lakini wakati huo huo anawaongoza wengi kwenye uharibifu. Kutokuwa na kiasi kunazipindua akili; kunaendekeza tamaa ya mwili, migogoro, na umwagaji damu unafuatia. Vita vinachochea tamaa mbaya za nafsi na kuwafagilia mbali wahanga wake milele na kuwatumbukiza kwenye uovu na umwagaji wa damu. Ni kusudi la Shetani kuyachochea mataifa kwenda vitani kwani kwa njia hiyo anaweza atawapotosha watu ili wasifanye Maandalizi ya kusimama katika siku ya hukumu.TK 356.3

  Shetani amejifunza siri za maumbile, na anatumia uwezo wake wote kudhibiti viumbe vya asili kwa kadiri Mungu anavyoruhusu. Ni Mungu anayewalinda viumbe wake dhidi ya mharabu. Hata hivyo, ulimwengu wa Kikristo umeonesha dharau kwa sheria yake ,na Bwana atafanya kile alichosema kuwa angekifanya - kuuondoa ulinzi wake kwa wale wanaoiasi sheria yake na kuwawalazimisha wengine kufanya hivyo. Shetani ndiye anayewadhibiti wale wote ambao kwa namna ya pekee hawalindwi na Mungu. Atawapatia upendeleo na ustawi baadhi yao, na ataleta shida kwa wengine, na kuwaongoza watu kuamini kuwa ni Mungu anayewatesa.TK 356.4

  Huku akijitokeza kama tabibu mkuu awezaye kuyaponya maradhi yao yote, Shetani ataleta magonjwa na majanga hadi miji yenye watu wengi itakapoharibiwa na kuwa magofu. Katika ajali za baharini na za nchi kavu, katika majanga makubwa ya moto, katika vimbunga vikali, na mvua za mawe, tufani, mafuriko, mawimbi ya bahari na matetemeko ya ardhi kwa namna mbalimbali; Shetani anautumia uwezo wake. Anayafagilia mbali mavuno yaliyokwisha kukomaa, kisha njaa na mateso vinafuata. Anaichafua hewa kwa harufu ya kufisha na watu wengi wanakufa.TK 357.1

  Kisha mwongo mkuu atashawishi watu kuelekeza mashtaka yao yote kwa wale ambao utii wao kwa shcria za Mungu ni shutuma ya daima kwa watenda dhambi. Itatamkwa kwamba watu wanamkosea Mungu kwa kuihalifu Jumapili, na kuwa dhambi hii imeleta maafa ambayo hayatakoma mpaka ushikaji wa Jumapili utakapolazimishwa. “Wale ambao wanaiharibu heshima ya Jumapili wanazuia urejeshwaji wa fadhila za mbinguni na ustawi.” Kwa hiyo shutuma za zamani dhidi ya mtumishi wa Mungu zitajirudia. “Ikawa, Ahabu alipomwona Eliya,.. Ahabu akamwambia, Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli?” 1 Fal. 18:17,18.TK 357.2

  Uwezo utendao miujiza utatumia mvuto wake dhidi ya wale wanaomtii Mungu kuliko wanadamu. “roho” watatamka kuwa Mungu amewatuma kuwashawishi wanaoipinga Jumapili juu ya kosa lao. Watalalamikia uovu mkubwa unaotendeka duniani na kuunga mkono shuhuda za walimu wa kidini kwamba uporomokaji wa maadili unasababishwa na kutoiheshimu Jumapili.TK 357.3

  Chini ya utawala wa Kanisa la Roma, wale walioteseka kwa sababu ya Injili walishutumiwa kuwa ni watenda maovu wakishirikiana na Shetani. Hivyo ndivyo itakavyokuwa sasa. Shetani atawasababisha wale wanaozitii sheria za Mungu washitakiwe kuwa ndio watu wanaoleta hukumu duniani. Kwa kutumia vitisho anajitahidi kutawala dhamiri za watu, akishawishi mamlaka za kidini na serikali kulazimisha sheria za binadamu zinazopingana na sheria ya Mungu.TK 357.4

  Wale wanaoiheshimu Sabato ya Biblia watashutumiwa kuwa ni adui wa sheria na utaratibu, kwamba wanavunja sheria za maadili, kusababisha vurugu na uharibifii, na kuleta hukumu ya Mungu duniani. Watashtakiwa kwa kuichukia serikali. Wachungaji wanaokana majukumu ya sheria ya mbingu watahubiri kutoka mimbarani jukumu la utii kwa mamlaka za kiraia. Katika kumbi za mabunge na katika mahakama za sheria, washika sheria watahukumiwa. Kauli zao zitapotoshwa; nia zao zitawasilishwa vibaya.TK 357.5

  Maafisa wakuu kutoka serikali na kanisani wataungana kuwashawishi au kuwalazimisha watu wote waiheshimu Jumapili. Hata ndani ya Marekani iliyo huru watawala na wabunge watalikubali hitaj linalopendelewa la sheria inayoshinikiza ushikaji wa Jumapili. Uhuru wa dhamiri ambao umegharimu kafara kubwa sana hautaheshimiwa tena. Katika Mgogoro unaokuja hivi karibuni tutaona mifano ya maneno kama yale ya nabii yakiigizwa . . . “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Ufu. 12:17TK 358.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents