Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushindi Waonekana Mapema

    Ndani ya gereza lake shimoni, aliuona mbeleni ushindi wa imani ya kweli. Katika njozi zake alimuona Papa na maaskofu wakifutilia mbali picha za Kristo alizokuwa amezichora kwenye kuta za kanisa dogo pale Prague. “Njozi ilimnyima raha : lakini siku iliyofuata aliona wachoraji wengi wakishughulika katika kurejesha picha hizi kwa wingi zaidi na katika rangi zilizong’aa zaidi...Wachoraji, ...wakiwa wamezingirwa na umati mkubwa, walisema kwa uchungu, ‘Sasa acha Mapapa na maaskofu waje; hawataweza kuzifuta zaidi!’” Mwanamatengenezo akasema, “Sura ya Kristo haitafutwa kamwe. Wametamani kuiharibu, lakini itachorwa upya kwenye mioyo yote kupitia kwa wahubiri wazuri kuliko mimi.” 21D’Aubigne, bk. l,ch. 6.TK 69.2

    Kwa mara ya mwisho, Huss aliletwa mbele ya baraza, kusanyiko kubwa la watu wenye akili-wafalme, watoto wa kifalme, wasaidizi wa mfalme, makadinali, maaskofu, mapadre, na umati mkubwa wa watu.TK 69.3

    Alipoulizwa atoe uamuzi wake wa mwisho, Huss alitamka kuwa asingekana msimamo wake. Huku akimkazia macho mfalme ambaye neno lake zito lilikuwa limekiukwa bila aibu, alisema, “Niliazimu, kwa kupenda kwangu mwenyewe, kusimama mbele ya baraza hili, nikiwa katika ulinzi wa umma na nia njema ya mfalme aliyeko hapa.” 22Bonnechose, vol 2, p. 84. Msisimko wa hisia kali ulionekana usoni mwa Sigismund wakati macho ya wote yalipomwelekea.TK 69.4

    Hukumu ilipotangazwa, utaratibu dhalili ulianza. Kwa mara nyingine akaitwa kufuta kauli yake, Huss akajibu, akigeukia watu: “Niitazame mbingu nikiwa na uso gani? Nitazameje ule umati wa watu ambao kwao nimehubiri Injili iliyo safi? La; ninaheshimu wokovu wao kuliko mwili huu dhaifu, ambao sasa unaelekezwa kwa mauti.” Mavazi ya upadre yaliondolewa moja baada ya jingine, kila askofu akitamka Iaana alipokuwa akifanya sehemu yake ya sherehe hii. Hatimaye, “walimwekea kichwani kofia ya kiaskofu ya karatasi iliyoundwa mfano wa piramidi, ambayo ilikuwa imechorwa picha za kutisha za maShetani, na kuandikwa maneno yaliyoonekana vizuri mbele ya kofla ‘Mzushi Mkuu’ . Huss akasema, ‘Kwa furaha sana, nitaivaa hii taji ya aibu kwa ajili yako, Ee Yesu, ambaye kwa ajili yangu uliivaa taji ya miiba.’ “ 23Wylie, bk. 3, ch. 7.TK 70.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents