Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kazi ya Luther Vaanza

    Sauti ya Luther ilisikika kutoka mimbarani ikiwa na onyo thabiti. Aliweka wazi mbele ya watu tabia ya hatia ya dhambi na alifundisha kuwa haiwezekani mwanadamu kupunguza hatia au kuepuka adhabu kwa matendo yake. Hakuna chochote kinachoweza kumwokoa mwenye dhambi isipokuwa toba kwa Mungu na imani kwa Kristo. Neema ya Kristo hainunuliwi; ni karama ya bure. Aliwashauri watu wasinunue vyeti vya msamaha, bali wamtafute kwa imani Mwokozi aliYesulubiwa. Aliwasimulia maumivu yake aliyokuwa ameyapitia na kuwahakikishia wasikilizaji wake kuwa kwa kumwamini Kristo alikuwa amepata amani na furaha.TK 84.1

    Kadiri Tetzel alivyoendelea kutoa maagizo yake yasiyomheshimu Mungu na wanadamu, Luther aliamua kuleta upinzani wenye nguvu zaidi. Kanisa la Wittenberg lilikuwa linamiliki vitu vya kumbukumbu ambavyo katika baadhi ya siku takatifu vilioneshwa kwa watu. Msamaha kamili wa dhambi ulitolewa kwa wote waliofika kanisani na kufanya maungamo. Moja kati ya matukio muhimu sana, siku kuu ya Watakatifu Wote, ilikuwa inakaribia. Luther, akiungana na makundi ya watu ambao tayari walikuwa wakienda kanisani, alibandika kwenye mlango maoni tisini na matano (95) dhidi ya fundisho la vyeti vya msamaha.TK 84.2

    Maoni yake yalileta mvuto mahali pote. Yalisomwa na kurudiwa kila upande. Kulitokea msisimko mkubwa katika mji mzima. Kwa Maandiko haya, ilioneshwa kwamba uwezo wa kutoa msamaha wa dhambi na kuondoa adhabu yake haukuwahi kutolewa kwa Papa au mwanadamu yeyote. Ilioneshwa kwa usahihi kuwa neema ya Mungu inatolewa bure kwa wote wanaoitafuta kwa toba na imani.TK 84.3

    Maandiko ya Luther yalisambaa katika nchi yote ya Ujerumani na ndani ya majuma machache yalikuwa yanasikika katika Ulaya nzima. Washiriki wengi waaminifu wa Kanisa la Roma walikuwa wanayasoma maoni hayo kwa furaha, wakiitambua ndani yake sauti ya Mungu. Walihisi kuwa Bwana alikuwa ameweka mkono wake ili kulituliza wimbi la uovu lililoumuka kutoka Roma. Wakuu na mahakimu walifurahi mioyoni mwao kwani mamlaka yenye kiburi, iliyokuwa imekataa maoni katika maamuzi yake, ingedhibitiwa.TK 84.4

    Walipoona kuwa mapato yao yalikuwa yanahatarishwa, mapadre werevu walighadhabika. Sasa Mwanamatengenezo huyu alikuwa anakabiliwa na washitaki wakali. Luther alijibu, “Ni nani asiyejua kuwa ni mara chache mtu huleta wazo jipya pasipo... kushitakiwa kwa kuchochea mafarakano?... Ni kwa nini Kristo na wafia-dini wote waliuawa? Kwa sababu... waliendeleza mambo mapya pasipo kunyenyekea na kupata mashauri ya mitazamo ya kale.” 47Ibid., ch. 6.TK 85.1

    Mbinu walizotumia maadui wa Luther, upotoshaji wa makusudi yake, na chuki waliyotumia kuelezea tabia yake, vilimjia kama mafuriko. Alipata ujasiri kuwa viongozi wangeungana naye kwa furaha kwenye matengenezo. Kwa subira aliiona siku yenye nuru ikipambazuka kwa ajili ya kanisa.TK 85.2

    Lakini badala ya kutiwa moyo alipokea shutuma. Viongozi wengi wa kanisa na serikali mara moja waliona kuwa kuzikubali hizi kweli, ingekuwa ni kushusha mamlaka ya Kanisa la Roma, kufunga maelfu ya mito iliyokuwa inatiririka kuelekea kwenye hazina, na hivyo kukatisha anasa za viongozi wa utawala wa Papa. Kuwafundisha watu wamtazame Kristo pekee kwa ajili ya wokovu ingekuwa ni kuipindua enzi ya Mapapa na hatimaye kuyaangamiza mamlaka yao wenyewe. Kwa hiyo walijipanga wenyewe kinyume na Kristo na ukweli kwa kumpinga mtu aliyemtuma kuwapa nuru.TK 85.3

    Luther alipojitazama mwenyewe alitetemeka - mtu mmoja anapingana na mamlaka zenye nguvu za dunia. Anaandika “Mimi nilikuwa nani kuupinga utukufu wa Papa, ambaye mbele zake...wafalme wa dunia na ulimwengu wote unatetemeka?... Hakuna mmoja awezaye kujua moyo wangu ulivyoteseka katika miaka hii miwili ya kwanza na ni katika huzuni kiasi gani, naweza kusema ni kukosa tumaini kwa namna gani, nilikuwa nimezama.” 48Ibid. Lakini msaada wa wanadamu uliposhindwa, alimtazama Mungu peke yake. Angeweza kujiegesha kwa usalama kwenye ule mkono wenye nguvu.TK 85.4

    Luther alimwandikia rafiki yake kuwa: “Jukumu lako ni kuanza kwa sala...usitumaini chochote kutokana na matendo yako, kutokana na ufahamu wako: mtumaini Mungu pekee, na katika mvuto wa Roho wake.” 49Ibid., ch. 7. Hapa lipo somo la muhimu kwa wale wanaohisi kuwa Mungu aliwaita ili waupeleke kwa wengine ukweli muhimu wa wakati huu. Katika mapambano dhidi ya nguvu za uovu kunahitajika kitu fulani zaidi ya akili na hekima ya kibinadamu.TK 86.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents