Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Bwana Anamkemea Shetani

  Na kwa yule mshitaki anasema: “Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! hiki si kinga kilichotolewa motoni?” Zekaria 3:2. Kristo atawavisha wale waaminifu wake vazi la haki yake, ili awalete kwa Baba yake “Kanisa tukufu, lisilo na ila waia kunyanzi wala lo lote kama hayo.” Waefeso 5:27.TK 300.1

  Hivyo itakuwa imetimia kwa ukamilifu ile ahadi ya agano jipya: “Nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” “Katika siku hizo na wakati huo, asema Bwana, uovu wa Israeli utatafutwa, wala uovu hapana; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana” “Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu.” Yeremia 31:34; 50:20; Isaya 4:3.TK 300.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents