Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utimilifu wa Kuvutia wa Unabii

  Unabii huu ulitimia kwa namna ya ajabu katika historia ya Ufaransa wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa, mnamo mwaka 1793. “Ufaransa inasimama kuwa nchi pekee katika historia ya dunia kutangaza kupitia Bunge lake kwamba hakuna Mungu, ambalo liliwafanya wakazi wote wanawake kwa wanaume wa mji mkuu na wengine wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini humo, kwa kulipokea tangazo hilo kwa kucheza na kuimba kwa furaha.” 170Blackwood Magazine, November, 1870..TK 174.3

  Ufaransa ilionesha tabia zilizokuwa zinadhihirishwa Sodoma. Mwanahistoria anatambulisha ukanamungu na ufuska wa Ufaransa kwa maneno haya: “Jambo lililokuwa limefungamana kwa karibu zaidi na sheria hizi zilizokuwa zinaathiri dini, lilikuwa ni lile lililodhalilisha uhusiano wa ndoa-uhusiano mtakatifu mwanadamu anaoweza kuufanya, na uthabiti wake ambao huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuimarisha jamii-na kuifanya mkataba wa muda mfupi, watu wowote wawili kuuingia na kuachana kimchezo mchezo...Mwigizaji maarufu wa vichekesho, Sophie Amoult; aliielezea ndoa ya aina hiyo kuwa ni ‘sakramenti ya uzinifu.” 171Sir Walter Scott, Life of Napoleon, Vol. 1, ch. 17.TK 174.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents