Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Prague Yawekwa Kwenye Katazo

    Habari zilipelekwa Roma, na Huss aliitwa ili asimame mbele za Papa. Kutii kungepelekea yeye kuuawa bila ya shaka. Mfalme na malkia wa Bohemia, Chuo Kikuu, waungwana, na maofisa wa serikali, waliungana katika mwito kwa Askofu Mkuu wa Roma kwamba Huss aruhusiwe kubaki Prague na kujibu kwa njia ya mjumbe. Badala yake, Papa aliendelea na kesi na kumhukumu Huss, kisha akautangaza mji wa Prague kuwa chini ya katazo.TK 65.2

    Wakati huu, hukumu hii ilisababisha mshtuko. Watu walimwangalia Papa kama mwakilishi wa Mungu, akishikilia funguo za mbinguni na kuzimu na akiwa na uwezo wa kuhukumu. Watu waliamini kuwa wafu walifungiwa nje ya makao ya amani hadi Papa alipoondoa amri ya kuwazuia. Huduma zote za kidini zilisitishwa. Makanisa yalifungwa. Huduma za ndoa zilifanyikia kwenye viwanja vya makanisa. Wafu walizikwa bila huduma kwenye mitaro au mashamba.TK 65.3

    Mji wa Prague ulijazwa na makelele. Kundi kubwa la watu lilimshutumu Huss na kudai apelekwe Roma. Ili kuituliza dhoruba, Mwanamatengenezo alijiondoa kwa muda na kwenda kijijini kwake alikozaliwa. Hakukoma kufanya kazi zake, lakini alisafiri ndani ya nchi akihubiri kwa makundi yaliyokuwa na shauku. Wakati msisimko wa Prague ulipopoa, Huss alirejea na kuendelea kuhubiri Neno la Mungu. Adui zake walikuwa na nguvu, lakini malkia na waungwana wengine wengi walikuwa rafiki zake, na idadi kubwa ya watu ilipelekana naye.TK 65.4

    Huss alikuwa amesimama mwenyewe katika kazi zake. Sasa Jerome alijiunga katika matengenezo. Hawa wawili waliungana katika maisha yao baada ya hapa, na katika kifo hawangetenganishwa. Katika zile sifa ambazo hufanya nguvu ya kweli ya tabia, Huss alikuwa mkuu zaidi. Jerome, akiwa na unyenyekevu wa kweli, alielewa thamani yake na kukubali mashauri yake. Wakiwa katika kutenda kazi pamoja matengenezo yaliendelea kwa haraka. Mungu aliruhusu nuru kuu kung’aa kwenye mawazo ya watu hawa wateule, akiwafunulia makosa mengi ya Kanisa la Roma, lakini hawakupokea nuru yote ambayo ilikuwa itolewe duniani. Mungu alikuwa akiwaongoza watu kutoka katika giza la Kanisa la Roma, na aliwaongoza, hatua kwa hatua, kadiri walivyoweza kuipokea. Kama ambavyo nuru ya jua la utosini iwezavyo kuwa kwa wale ambao wamekaa gizani kwa muda mrefu, mwanga wote ungesababisha wageukie mbali. Kwa sababu hiyo, aliifunua hatua kwa hatua, kwa kadiri ilivyoweza kupokelewa na watu.TK 65.5

    Utengano kanisani uliendelea. Mapapa watatu walikuwa wakishindania ukuu. Ugomvi wao ulijaza vurugu katika Ukristo. Bila kuridhika na tabia ya kutupiana laana, kila mmoja alijitosa katika kununua silaha na kuwa na askari. Bila shaka ilikuwa ni lazima kuwa na fedha; ili kupata hivi, zawadi, ofisi na baraka za kanisa zilitolewa kwa kuuzwa. (Angalia Kiambatisho.)TK 66.1

    Kwa ujasiri ambao ulikuwa ukiongezeka, Huss alitoa shutuma dhidi ya machukizo yaliyokuwa yakivumiliwa katika jina la dini. Watu walilikosoa Kanisa la Roma hadharani kwamba lilikuwa chanzo cha mateso yaliyokuwa yanaugubika Ukristo.TK 66.2

    Kwa mara nyingine Prague ilionekana ikiwa katika ukingo wa pambano la damu. Kama ilivyokuwa wakati wa zama zilizopita, mtumishi wa Mungu alishtakiwa kama “mtaabishaji wa Israeli.” 1 Fal. 18:17. Mji uliwekwa tena chini ya katazo, na Huss akatoka tena kwenda kwenye kijiji chake alikozaliwa. Alikuwa azungumze tena kwa watu wengi, kwa Wakristo wote, kabla ya kukabidhi uhai wake chini kama shahidi wa ukweli.TK 66.3

    Baraza kuu liliitishwa ili kukutana pale Constance (Kusini Magharibi mwa Ujerumani), ambalo liliitishwa kutokana na matashi ya mfalme Sigismund na pia mmoja kati ya Mapapa watatu waliokuwa wakishindana, Yohana XXIII. Papa Yohana, ambaye tabia na sera zake visingeweza kufaa hata kuchunguzwa, hakuweza kudiriki kumpinga Sigismund. (Angalia Kiambatisho.)TK 66.4

    Makusudi makuu ambayo yalikuwa yafikiwe ni kuponya utengano katika kanisa na kuung’oa “uzushi.” Hawa Mapapa wawili waliopingana waliitwa kuhudhuria pamoja na John Huss. Mapapa waliwakilishwa na wajumbe wao. Papa Yohana alikuja akiwa na mashaka makubwa, akihofu kuhojiwa kwa ajili ya maovu ambayo yalikuwa yamedhalilisha taji, pamoja na uhalifu uliotumika kuitunza. Hata hivyo aliingia mjini Constance kwa fahari kubwa, akisindikizwa na msafara wa watumishi wa mahakama. Juu ya kichwa chake kulikuwa na mfuniko wa dhahabu, uliobebwa na mahakimu wakuu wanne. Mkate wa Bwana ulikuwa umebebwa mbele yake, na mavazi ya kitajiri ya makadinali na waungwana yalifanya mwonekano uwe wa kuvutia.TK 66.5

    Wakati huo huo msafiri mwingine alikuwa anakaribia Constance. Huss aliachana na marafiki zake kana kwamba asingeonana nao tena, akihisi kuwa safari yake ilikuwa iishie kwenye kuchomwa moto. Alikuwa amepewa hati ya usalama wakati wa kusafiri kutoka kwa mfalme wa Bohemia vile vile nyingine kutoka kwa Mfalme Sigismund. Lakini alifanya maandalizi yote katika mtazamo wa uwezekano wa kifo chake.TK 67.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents