Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Muungano wa Upagani na Ukristo

    Kitendo cha Kanisa Katoliki la Roma, kuunganisha upagani na Ukristo, na kama ulivyo upagani, kupotosha tabia ya Mungu; kimepelekea vitendo vya ukatili mkubwa. Vyombo vya mateso viliwalazimisha watu wakubali mafundisho yake. Watu wenye vyeo kanisani walijifunza kuvumbua njia za kusababisha mateso makali iwezekanavyo bila kuwaua wale waliokataa kuyakubali madai yake. Katika matukio mengi, mtu aliyekuwa anateseka alikikaribisha kifo kama pumziko tamu.TK 346.2

    Kwa wafuasi wake waaminifu, Kanisa la Roma lilikuwa linatumia adhabu za mijeledi, kuwanyima chakula, na nyingine za kimwili. Ili kupata kibali cha mbinguni, wenye kutubu walifundishwa kujitenga na vifungo alivyoweka Mungu ili awabariki na kuwapa furaha kama wapitaji duniani. Uwanja wa kanisa umejaa mamilioni ya watu ambao katika maisha yao wanafanya jitihada zisizo na mafanikio, za kuzuia kila wazo na hisia ya huruma kwa viumbe wenzao kana kwamba mambo hayo yanamchukiza Mungu. Mungu hawabebeshi wanadamu mizigo hiyo mizito. Kristo hakuweka kielelezo kwa wanaume na wanawake kujifungia kwenye nyumba za watawa ili wastahili kuingia mbinguni. Hakufundisha kuwa upendo ni lazima unyamazishwe.TK 346.3

    Papa anadai kuwa yeye ni wakili Wakristo. Lakini, je, kuna tukio lolote linaloonesha kuWakristo alikuwa anawafunga watu gerezani kwa kosa la kutomsheshimu kama mfalme wa mbinguni? Je, sauti yake ilisikika ikiwahukumu kifo wale waliokuwa wamemkataa?TK 346.4

    Kanisa Katoliki linajionesha mbele ya ulimwengu kuwa linatenda haki, huku likiomba radhi na kuzifunika kumbukumbu za ukatili wake wa kutisha. Limejivika mavazi kama ya Kristo, lakini halijabadilika. Kila kanuni ya zamani ya utawala wa Papa ipo hadi leo. Mafundisho yaliyobuniwa zama za giza bado yanashikiliwa hadi leo. Utawala wa Papa ambao Waprotestanti wa leo wanauheshimu ni ule ule uliokuwa unatawala katika siku za Wanamatengenezo, wakati watu wa Mungu waliposimama ili kuufunua uovu wake wakihatarisha maisha yao.TK 347.1

    Utawala wa Papa uko vile ulivyo sawa na unabii ulivyotamka, kwamba kungekuwa na uasi ambao ungekuja baadaye. 2Wathesalonike 2:3, 4. Chini ya mwonekano wa kinyonga unaobadilika, utawala wa Papa umeifunika sumu ya nyoka isiyobadilika. Je, nguvu hii, ambayo kumbukumbu yake kwa miaka elfu moja, imeandikwa kwa damu ya watakatifu; sasa ikubaliwe kama sehemu ya kanisa la Kristo?TK 347.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents