Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kujifunza Biblia Kila Mahali

    Wakati wa usiku walimu wa shule za vijijini waliyasomea kwa sauti makundi madogo ya watu waliokuwa wamekusanyika kwenye sebule za kuotea moto. Kwa kila jitihada baadhi ya watu; walisadikishwa ukweli. “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.” Zaburi 119:130.TK 126.2

    Wafuasi wa Kanisa la Papa waliokuwa wamewaachia makasisi na watawa jukumu la kujifunza Maandiko; sasa waliwaita ili wayakanushe mafundisho mapya. Lakini, kwasababu ya kutojua kwao Maandiko, makasisi na watawa walishindwa kabisa. Mwandishi mmoja Mkatoliki alisema, “Kwa majonzi makubwa, Luther amewashawishi wafuasi wake kutoamini hekima yoyote isipokuwa Maandiko Matakatifu.” 116Ibid. Makundi ya watu yalikusanyika kusikia ukweli uliokuwa ukitolewa na watu waliokuwa na elimu ndogo. Ujinga wenye kuaibisha wa wakuu ulidhihirika kwa hoja zao kujibiwa na mafundisho sahili kutoka katika Neno la Mungu. Wafanyakazi, askari, wanawake na hata watoto walikuwa na uelewa mpana wa Maandiko kuliko makasisi na madaktari waliofuzu.TK 126.3

    Vijana wenye nia kuu walijitoa kujifunza, wakiyachunguza Maandiko na kujizoeza juu ya kazi za kale zilizoandikwa kwa ustadi. Wakiwa na akili zinazofanya kazi vizuri na bila mioyo ya hofu, vijana hawa walipata elimu ambayo kwa kipindi kirefu mtu yeyote asingeweza kushindana nayo. Katika mafundisho mapya, watu walikuwa wamepata mambo yaliyokidhi mahitaji ya mioyo yao, na waliwapa kisogo wale ambao, kwa muda mrefu, waliwalisha makapi yasiyofaa ya sherehe za mapokeo potovu na desturi za kibinadamu.TK 126.4

    Mateso yalipochochewa dhidi ya walimu wa ukweli, waliyakumbuka maneno ya Kristo: “Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine,” Mathayo 10:23. Wakimbizi wangeweza kupata hifadhi na kukaribishwa na watu wakarimu, na kwa hiyo wangemhubiri Kristo pengine kanisani ama katika nyumba za watu binafsi au mahali pa wazi. Ukweli uliendelea kusambaa bila kipingamizi chochote.TK 127.1

    Viongozi wa kanisa na serikali, bila mafanikio, waliwafunga gerezani, mateso, moto na upanga. Maelfu ya waumini walitia muhuri imani zao kwa damu yao, na bado mateso yalisaidia tu kueneza ukweli. Itikadi kali ambazo Shetani alijaribu kuungana nazo; zilileta matokeo dhahiri ya tofauti iliyokuwepo kati ya kazi ya Shetani na kazi ya Mungu.TK 127.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents