Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Picha Mbili Zamvutia Huss

  Katika kipindi hiki, wageni wawili kutoka Uingereza, wasomi, walikuwa wamepokea nuru na walikuwa wamekuja kuisambaza mjini Prague. Walinyamazishwa baada ya muda mfupi, lakini kwa sababu hawakuwa tayari kuacha kusudi lao, walihamia kwenye mbinu nyingine. Hali wakiwa wasanii pamoja na kuwa wahubiri, walichora picha mbili mahali palipokuwa wazi. Moja iliwakilisha kuingia kwa Kristo Yerusalemu, “Mpole, naye amepanda punda” (Mt.21:5) akifuatwa na wanafunzi wake waliovaa mavazi yaliyochakazwa na safari na miguu isiyo na viatu. Picha nyingine ilionesha msafara wa Papa-Papa katika mavazi yake ya kifahari na taji yenye ngazi tatu, akiwa juu ya farasi huku akiwa amepambwa kwa uzuri wa ajabu, akitanguliwa na wapiga tarumbeta na kufuatiwa na makadinali na maaskofu waliovalia mavazi yanayong’aa.TK 64.3

  Umati wa watu walikuja kuangalia michoro hii. Hakuna aliyeshindwa kupata ujumbe uliokuwamo kwenye michoro. Kukawa na ghasia kubwa Prague, na wale wageni wakaona kuwa ilikuwa muhimu waondoke. Lakini picha hizi ziliweka mvuto mkali ndani ya Huss na kumuongoza kujifunza Biblia zaidi na pia maandishi ya Wycliffe.TK 64.4

  Ingawa alikuwa bado hajajiandaa kukubali matengenezo yote yaliyopiganiwa na Wycliffe, aliona tabia ya kweli ya utawala wa Papa, na akashutumu kiburi, tamaa ya makuu na upotovu wa mamlaka ya Papa.TK 65.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents