Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Tyndale Atafsiri Agano Jipya kwa Kiingereza

  Mateso yalimlazimisha Tyndale kukimbia nyumbani na kwenda London alikofanya kazi bila kubughudhiwa kwa kipindi fulani. ICwa mara nyingine tena wafuasi wa Kanisa la Roma walimlazimisha kukimbia. Ilikuwa inaonekana kwamba Uingereza yote ilikuwa haihitaji kumpokea. Kule Ujerumani alianza kuchapa Agano Jipya kwa lugha ya Kiingereza. Alipokatazwa kuchapa katika mji mmoja alikwenda kwenye mji mwingine. Hatimaye alifika mji wa Worms, mahali ambapo miaka michache kabla yake, Luther alikuwa ameitetea Injili mbele ya baraza la kidini. Kwenye mji huo marafiki wa imani ya Matengenezo walikuwa wengi. Hapa kwa kipindi kifupi nakala elfu tatu za Agano Jipya zilikamilika, na toleo lingine lilifuata.TK 160.3

  Neno la Mungu lilisafirishwa kwa siri kwenda London na kusambazwa katika nchi nzima. Wafuasi wa Kanisa la Roma walijaribu kuukandamiza ukweli bila ya mafanikio. Askofu wa Durham alinunua nakala zote za Biblia toka kwa mwuza vitabu kwa nia ya kwenda kuziharibu, akidhania kwamba jambo hilo lingekwamisha kazi. Pesa hiyo iliyokuwa imetolewa ilinunua mali ghafi kwa toleo jipya na bora zaidi. Baadaye Tyndale alipokuwa amefungwa, aliahidiwa kuachiliwa huru kwa sharti moja, ataje majina ya waliokuwa wamemsaidia kugharimia uchapaji wa Biblia.TK 160.4

  Alijibu kuwa askofu wa Durham alikuwa amechangia pesa nyingi kuliko mtu mwingine yoyote kwa kununua Biblia zilizokuwa zimebaki kwa bei kubwa.TK 161.1

  Hatimaye Tyndale aliishuhudia imani yake kwa kifo cha mfia dini; lakini silaha alizokuwa ameziandaa ziliwasaidia askari wengine kupigana vita kwa kame nyingi, mpaka katika wakati wetu.TK 161.2

  Kutoka katika mimbari, Latimer aliendelea kusema kwamba, Biblia inapaswa isomwe na watu kwa lugha yao. “Hebu tusiiache njia, lakini turuhusu Neno la Mungu lituongoze: wala tusienende... kama mababu zetu, wala tusiache kutafuta kujua walichokuwa wanafanya, lakini pia kile walichokuwa wanatakiwa kufanya.” 159Hugh Latimer, “First Sermon Preached Before King Edward VI.”TK 161.3

  Viongozi wa imani ya Matengenezo nchini Uingereza, Bames na Frith, Ridley na Cranmer walikuwa wasomi walioheshimika sana kwa juhudi zao ama kicho chao kwa Mungu kwenye jamii ya waumini wa Kanisa la Roma. Upinzani wao kwa utawala wa Papa yalikuwa ni matokeo ya ufahamu wao kuhusu makosa ya “Mamlaka ya Papa.”TK 161.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents