Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Fundisho Potovu la Mateso ya Milele

    Uovu umeletwa na fundisho potovu la mateso ya milele. Dini ya Biblia, iliyojaa upendo na wema imetiwa giza kwa mapokeo potovu na kufunikwa na vitisho. Shetani ameipotosha tabia ya Mungu. Mwumbaji wetu mwenye rehema anaogopwa, anahofiwa, na hata kuchukiwa. Mitazamo ya Mungu anayeogofya iliyosambaa kote duniani kutokana na mafundisho ya kwenye mimbara; imewafanya watu wengi kuwa na mashaka na makafiri.TK 329.3

    Mateso ya milele ni moja ya mafundisho ya uongo, mvinyo wa machukizo (Ufunuo 14:8; 17:2), ambao Babeli anayanywesha mataifa. Watumishi Wakristo waliukubali uasi huu kutoka Kanisa la Roma kama walivyokuwa wameipokea sabato ya uongo. Kama tukiliacha Neno la Mungu na kuyakubali mafundisho ya uongo kwa vile baba zetu waliyafundisha, tunaangukia kwenye hukumu iliyotangazwa juu ya Babeli; tunakunywa mvinyo wa machukizo yake.TK 329.4

    Kundi kubwa la watu wamevutwa kuelekea kwenye kosa lililo kinyume. Wanaona kuwa Maandiko yanamwakilisha Mungu kuwa ni mwenye upendo na huruma na hawaamini kuwa atawapeleka viumbe wake kwenye moto wa milele. Wanashikilia fundisho kuwa roho kwa asili ina hali ya kutokufa; wanahitimisha kuwa wanadamu wote wataokolewa. Kwa hiyo mwenye dhambi anaweza kuishi kwa anasa za ubinafsi, akipuuza matakwa ya Mungu, na bado akapokelewa naye. Fundisho la aina hii, linalotambua rehema ya Mungu huku likipuuza haki yake; linafurahisha tamaa ya mwili.TK 329.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents