Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hawajajitayarisha Kuingia Mbinguni

    Wale ambao wamemchagua Shetani kuwa kiongozi wao, hawajajitayarisha kuingia kwenye uwepo wa Mungu. Majivuno, udanganyifu, tamaa ya mwili, ukatili vimekazwa katika tabia zao. Je, wanaweza kuingia mbinguni na kuishi milele na wale ambao waliwachukia duniani? Ukweli hautakubalika kwa mtu mwongo, upole hautakidhi haja ya kujitukuza nafsi; usafi haukubaliki kwa mtoa rushwa; upendo usiotaka faida haumvutii mbinafsi. Ni fursa gani ambayo mbingu zingetoa kwa wale ambao wametopea kwenye matakwa ya ubinafsi?TK 332.1

    Je, wale ambao mioyo yao imejazwa na chuki kwa Mungu, na wanaochukizwa na ukweli na utakatifu, wataweza kuchangamana na umati wa mbinguni na kuimba pamoja nyimbo za sifa? Walipewa miaka ya matarajio lakini, hawakuzifunza akili zao kupenda usafi. Hawakujifunza lugha ya mbinguni. Na sasa wamechelewa.TK 332.2

    Maisha ya uasi dhidi ya Mungu yamewakosesha kuingia mbinguni. Utakatifu na amani yake vitakuwa ni mateso kwao; utukufu wa Mungu utakuwa ni moto ulao. Watatamani kukimbia kutoka ile sehemu takatifu, na wataomba uharibifu uwafike, ili angalau wasiuone uso wa Yeye aliyekufa ili awakomboe. Hatima ya waovu inapangwa kutokana na uchaguzi wao. Kutokuwepo kwao mbinguni ni hiari yao, na ni haki na rehema kwa upande wa Mungu. Kama yalivyo maji ya mafuriko, moto wa siku ile kuu unatangaza hukumu ya Mungu kwamba waovu hawatapona. Mapenzi yao waliyatimiza katika uasi. Uhai utakapokuwa umekoma, wamechelewa, hawawezi kuyageuza mawazo yao kutoka kwenye uasi kwenda kwenye utii, kutoka kwenye chuki kwenda kwenye upendo.TK 332.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents