Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 31 - Roho Za Uchafu

    Malaika wa Mungu na roho wachafu wamefunuliwa kwa uwazi ndani ya Maandiko Matakatifu na haiwezekani kuwatenganishana historia ya wanadamu. Malaika watakatifu, wanao “hudumu wale watakaourithi wokovu” (Waebrania 1:14) wanadhaniwa na wengi kuwa ni roho za wafu. Lakini Maandiko yanatoa uthibitisho kuwa hawa siyo roho zilizotengana na miili ya waliokufa.TK 315.1

    Kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu, malaika walikuwepo tayari, kwani wakati misingi ya ulimwengu ilipowekwa, “...nyota za asubuhi ziliimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipiga kelele kwa furaha.” Baada ya anguko la mwanadamu, malaika walitumwa kwenda kuulinda mti wa uzima kabla mwanadamu hajafa. Malaika wana nguvu kuliko wanadamu kwa sababu, mwanadamu alifanywa ... ” mdogo punde kuliko Mungu.” Zaburi 8:5TK 315.2

    Anasema nabii, “...nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi.” Mbele ya Mfalme wa wafalme wanasubiri- “Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake” “Mkiisikiliza sauti ya neno lake.” majeshi ya malaika elfu nyingi” Ufunuo 5:11; Zaburi 103:20,21; Waebrania 12:22. Kama wajumbe wa Mungu wanakwenda haraka, “kama kuonekana kwa kumulika kwa umeme.” Wanaruka haraka sana. Malaika aliyeonekana kwenye kaburi la Mwokozi, sura yake, “ilikuwa kama umeme”, ikasababisha walinzi kutetemeka kwa hofu na, “wakawa kama wafu.” Senakeribu alipomkufuru Mungu na kuwatishia Israeli, “malaika wa Bwana alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu.” Ezekieli 1:14; Mathayo 28:3,4; 2 Wafalme 19:35.TK 315.3

    Malaika hutumwa kwa ajili ya kuwarehemu watoto wa Mungu. Kwa Ibrahimu, walikwenda na ahadi ya baraka; Sodoma, kumwokoa Lutu kwenye maangamizi; kwa Eliya , aliyekuwa karibu kuangamia jangwani; kwa Elisha, wakiwa na magari ya farasi wa moto alipokuwa amezingirwa na adui zake; kwa Danieli, alipotupwa awe chakula cha simba; kwa Petro alipokabiliwa na kifo ndani ya gereza la Herode; kwa wafungwa kule Filipi; kwa Paulo, katika usiku wa dhoruba baharini; kwenda kufungua moyo wa Komelio ili apokee Injili; kumtuma Petro akiwa na ujumbe wa wokovu kwa mgeni mmataifa-hivyo malaika watakatifu waliwatumikia watu wa Mungu.TK 315.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents