Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu akageuza matokeo

  Wakati mkono wa Mungu ulionekana ukiwashota kuvuka bahari kwenda kwa inchi ambayo wanaweza kupata inchi na kuachia watoto wao uriti wa uhuru wa dini, wakaendelea katika njia ya maongozi ya Mungu. Mateso na kujihamisha vilikuwa vikifungua njia kwa uhuru.TSHM 136.6

  Wakati mara ya kwanza walipolazimishwa kujitenga kutoka kwa kanisa la Kiingereza, Watu walioishi maisha safi wakajiunga waowenyewe kwa maagano kama watu huru wa Bwana “kwa kutembea pamoja katika njia zake zote zilizojulishwa ao zinazopaswa kujulishwa kwao.” Hapa ndipo palikuwa na kanuni ya maana sana ya Kiprotestanti. Kwa kusudi hili Wasafiri wakatoka Uholandi kutafuta makao katika Dunia Mpya. Yohana Robinson, mchungaji wao, katika hotuba yake ya kuaga kwenda kwa mahamisho akasema:TSHM 136.7

  “Nawaagiza mbele ya Mungu na malaika wake wenye kubarikiwa kwamba munifuate si mbali kama nilivyomfuata Kristo. Kama Mungu angepashwa kufunua kitu cho chote kwenu kwa chombo kingine chake, muwe tayari kukikubali kwa furaha mliyokuwa nayo kukubali ukweli wa kazi yangu ya kuhubiri; kwa maana ninakuwa na tumaini kwamba Bwana anakuwa na ukweli zaidi na nuru kuangazia ya neno lake takatifu.”TSHM 137.1

  “Kwa upande wangu mimi, siwezi kusikitikia ya kutosha hali ya makanisa ya matengenezo, ambayo ...haitaenda sasa mbali zaidi kuliko wasimamizi wao wa matengenezo. Haiwezekani kuvuta watu wa dini ya Luther kufanya hatua moja zaidi mbali kuliko Luther alivyoona; ... na watu wa imani ya Calvin, munawaona wanabakia pale ambapo mutu mkuu wa Mungu aliwaacha, ambaye hata hivyo hakuona mambo yote. ... Ijapo walikuwa taa za kuwaka na kuangaza katika wakati wao, lakini hawakujua shauri lote la Mungu, lakini kama wangaliishi leo, wangekubali nuru mpya zaidi kama ile waliyokubali mara ya kwanza.”TSHM 137.2

  “Kumbukeni ahadi yenu na agano pamoja na Mungu na pamoja na mtu kwa mwenzake, kukubali nuru yo yote na ukweli utakaojulishwa kwenu kutoka kwa neno lake lililoandikwa; lakini zaidi, mjihazari, nawasihi, kuhusu mnayokubali kwa ajili ya kweli, na kuilinganisha na kupima uzito wake kwa maandiko mengine ya ukweli mbele ya kuikubali; kwani haiwezekani kwa dunia la Kikristo ambayo ilitoka giza nzito kwa kuchelewa ifikie maarifa kamili mara moja.”TSHM 137.3

  Haja ya uhuru wa zamiri ikaongoza Wasafiri kuvuka bahari, kuvumukia magumu ya jangwani, na kuweka msingi wa taifa kubwa. Lakini Wasafiri hawakufahamu bado kanuni ya uhuru wa dini. Uhuru ambao walijitolea kafara sana kwa ajili yao wenyewe, hawakuwa tayari kuutolea wengine. Mafundisho ambayo Mungu alitolea Kanisa haki ya kuongoza zamiri na kuleza wazi na kuazibu uzushi ni mojawapo ya makosa makubwa ya Kanisa la Roma. Watengenezaji hawakuwa na uhuru kabisa kwa roho ya Roma ya kutovumilia. Giza kubwa sana ambayo Roma ilifunika Kanisa la Kikristo haikuondolewa kabisa.TSHM 137.4

  Kanisa la serkali lilitengenezwa na wagandamizi, waamuzi walioruhusiwa kukomesha uzushi. Kwa hiyo uwezo wa serkali ulikuwa mikononi mwa Kanisa. Mipango hii haikuleta matokeo mengine isipokuwa mateso.TSHM 137.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents