Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maumivu Makuu ya Roho Sasa Yakalemea Juu ya Luther

    Wana wa wafalme wa upande wa Papa wakatangaza kwamba uasi ulikuwa tunda ya mafundisho ya Luther. Mzigo huu hakupashwa lakini kuleta huzuni kubwa kwa Mtengenezaji kwamba kisa cha kweli kilipaswa kuaibishwa kwa kuhesabiwa pamoja na ushupavu wa dini wa chini zaidi. Kwa upande mwengine, waongozi katika uasi walimchukia Luther. Hakukana madai yao kwa maongozi ya Mungu tu, bali akawatangaza kuwa waasi juu ya mamlaka ya serkali. Katika uhusiano wakamshitaki yeye kuwa mdai wa msingi.TSHM 88.3

    Roma ilitumainia kushuhudia muanguko wa Matengenezo. Na wakamlaumu Luther hata kwa ajili ya makosa ambayo alijaribu kwa bidii sana kusahihisha. Kundi la ushupavu, likadai kwa uongo kwamba lilitendewa yasiyo haki, wakapata huruma ya hesabu kubwa ya watu na kuzaniwa kuwa kama wafia dini. Kwa hiyo wale waliokuwa katika kupingana na Matengenezo wakahurumiwa na kusafishwa. Hii ilikuwa kazi ya roho ya namna moja ya uasi wa kwanza uliopatikana mbinguni.TSHM 88.4

    Shetani hutafuta kila mara kudanganya watu na kuwaongoza kuita zambi kuwa haki na haki kuwa zambi. Utakatifu wa uongo, utakaso wa kuiga, ungali ukionyesha roho ya namna moja kama katika siku za Luther, kugeuza mafikara kutoka kwa Maandiko na kuongoza watu kufuata mawazo na maono kuliko sheria za Mungu.TSHM 88.5

    Kwa uhodari Luther akatetea injili kwa mashambulio. Pamoja na Neno la Mungu akapigana juu ya mamlaka ya manyanganyi ya Papa, wakati aliposimama imara kama mwamba kupinga ushupavu uliojaribu kujiunga na Matengenezo.TSHM 88.6

    Pande zote za upinzanihuweka pembeni Maandiko matakatifu, kwa faida ya hekima ya kibinadamu kutukuzwa kawa chemchemi ama asili ya ukweli. Kufuata akili za kibinadamu kwa kusudi lakuabudu kama Mungu na kufanya hii kanuni kwa ajili ya dini. Kiroma kinadai kuwa na uongozi wa Mungu ulioshuka kwa mustari usiovunjika toka kwa mitume na kutoa nafasi kwa ujinga na uchafu vifichwe chini ya agizo la “mitume”. Maongozi yaliyodaiwa na Munzer yalitoka kwa mapinduzi ya mawazo. Ukristo wa kweli hukubali Neno la Mungu kama jaribio la maongozi yote.TSHM 88.7

    Kwa kurudi kwake Wartburg, Luther akatimiza kutafsiri Agano Jipya, na injili ikatolewa upesi kwa watu wa Ujeremani katika lugha yao wenyewe. Ufasiri huu ukapokewa kwa furaha kubwa kwa wote waliopenda ukweli.TSHM 89.1

    Wapadri wakashtushwa kwa kufikiri kwamba watu wote wangeweza sasa kuzungumza pamoja nao Neno la Mungu na kwamba ujinga wao wenyewe ungehatarishwa. Roma ikaalika mamlaka yake yote kuzuia mwenezo wa Maandiko. Lakini kwa namna ilivyozidi kukataza Biblia, ndivyo hamu ya watu ikazidi kujua ni nini iliyofundishwa kwa kweli. Wote walioweza kusoma wakaichukua kwao na hawakuweza kutoshelewa hata walipokwisha kujifunza sehemu kubwa kwa moyo. Mara moja Luther akaanza utafsiri wa Agano la Kale.TSHM 89.2

    Maandiko ya Luther yakapokewa kwa furaha sawasawa katika miji na katika vijiji. “Yale Luther na rafiki zake waliyoandika, wengine wakayatawanya. Watawa, waliposadikishwa juu ya uharamu wa kanuni za utawa, lakini wajinga sana kwa kutangaza neno la Mungu ... wakauzisha vitabu vya Luther na rafiki zake. Ujeremani kwa upesi ukajaa na wauzishaji wa vitabu wajasiri.”TSHM 89.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents