Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uchuuzi wa cheti cha Kuachiwa Zambi katika Usuisi

    Katika Ujermani biashara ya kuachiwa (zambi) iliongozwa na mwovu sana Tetzel. Katika Usuisi biashara hii ilikuwa chini ya uongozi wa Samson, mtawa wa Italia. Samson alikuwa amekwisha kujipatia pesa nyingi kutoka Ujeremani na Usuisi kwa kujaza hazina ya Papa. Sasa akapitia Usuisi, kunyanganya wakulima masikini mapato yao machache na kulipisha zawadi nyingi kutoka kwa watajiri. Mtengenezaji kwa upesi akaanza kumpinga. Kufanikiwa kwa Zwingli kulikuwa namna hiyo kufunua kujidai kwa mtawa huyu hata akashurutisha kutoka kwenda sehemu zingine. Huko Zurich, Zwingli akahubiri kwa bidii juu ya wafanya biashara ya msamaha. Wakati Samson alipokaribia mahali pale akakutana na mjumbe aliyemtetea neno kutoka kwa baraza kwa kumwaambia aanze kazi, akatumia mwingilio wa hila, lakini, akarudishwa bila kuuzisha hata barua moja ya msamaha, kwa upesi akatoka Usuisi.TSHM 82.1

    Tauni, au Kifo Kikubwa, kikapitia kwa Usuisi kwa nguvu sana katika mwaka 1519. Wengi wakaongozwa kuona namna ilikuwa bure na bila damani masamaha yaliokuwa wakinunua; wakatamani sana msingi wa kweli wa imani yao. Huko Zurich, Zwingli akagonjwa sana, na habari ikatangazwa sana kwamba alikufa. Kwa saa ile ya kujaribiwa akatazama kwa imani msalaba wa Kalvari, akatumaini kwamba kafara ya Kristo ilikuwa ya kutosha kwa ajili ya zambi. Aliporudi kutoka kwa milango ya mauti, ilikuwa kwa ajili ya kuhubiri injili kwa bidii kubwa sana kuliko mbele. Watu wao wenyewe walitoka kuangalia mgonjwa karibu ya kifo, wakafahamu vizuri kuliko mbele, damani ya injili.TSHM 82.2

    Zwingli alifikia hali ya kuelewa wazi juu ya ukweli na kupata ujuzi ndani yake uwezo wake unaogeuza. “Kristo,” akasema, “... alitupatia ukombozi wa milele ... mateso yake ni ... kafara ya milele, na huleta kupona kwa milele; huridisha haki ya Mungu kwa milele kwa ajili ya wale wote wanaotegemea juu ya kafara yake kwa imani ya nguvu na ya imara. ... Panapokuwa imani katika Mungu, kunakuwa na juhudi inayoendesha na kusukuma watu kwa kazi njema.”TSHM 82.3

    Hatua kwa hatua Matengenezo yakaendelea katika Zurich. Katika mushtuko adui zake wakaamka kwa kushindana kwa bidii. Mashambulio mingi yakafanywa juu ya Zwingli. Mwalimu wa wapinga imani ya dini anapashwa kunyamazishwa. Askofu wa Constance akatuma wajumbe watatu kwa Baraza la Zurich, kumshitaki Zwingli juu ya kuhatarisha amani na utaratibu wa jamii. Kama mamlaka ya kanisa ikiwekwa pembeni, akasema, machafuko kote ulimwenguni yatatokea.TSHM 82.4

    Baraza likakataa kukamata mpango juu ya Zwingli, na Roma ikajitayarisha kwa shambulio jipya. Mtengenezaji akapaliza sauti: “Muache waje”; Ninawaogopa kama vile mangenge yanayo tokajuu yakimbiavyo mavimbi yanayo mgurumo kwa miguu yake.” Juhudi za waongozi wa kanisa ziendelesha kazi waliotamani kuharibu. Kweli ikaendelea kusambaa. Katika Ujeremani wafuasi wake, walipohuzunishwa kwa kutoweka kwa Luther, wakatiwa moyo tena walipoona maendeleo ya injili katika Usuisi. Namna Matengenezo yaliimarishwa katika Zurich, matunda yake yalionekana zaidi kabisa katika kuvunjwa kwa uovu na kuendeleshwa utaratibu.TSHM 83.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents