Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kimya Kamili wa Agano Jipya

    Waprotestanti wanatambua “kimya kamili cha Agano Jipya kadiri hakuna agizo lo lote wazi kwa ajili ya Sabato (Jumapili, siku ya kwanza ya juma) wala kanuni halisi kwa kushikwa kwake zinazohusiana nayo.”TSHM 216.2

    “Hata kwa wakati wa kufa kwa Kristo, hakuna badiliko lililofanyika katika siku”; na “ni hivyo kama maandiko yanavyoonyesha, wao (mitume) ... hawakutoa agizo lo lote la wazi kuonyesha kuachwa kwa Sabato ya siku ya saba, na kushikwa kwake kwa siku ya kwanza ya juma.”TSHM 216.3

    Wakatoliki wa Roma wanatambua kwamba badiliko la Sabato lilifanywa na kanisa lao, na kutangaza kwamba Waprotestanti, kwa kushika Jumapili (siku ya kwanza ya juma), wanatambua mamlaka ya Roma. Maneno yamesemwa: “Wakati wa sheria ya kale, jumamosi (siku ya saba) ilikuwa siku iliyotakaswa; lakini kanisa, lilipoagizwa na Yesu Kristo, na kuongozwa na Roho ya Mungu, likabadilisha Jumapili (siku ya kwanza ya juma: Dimanche) kwa Jumamosi (siku ya saba ya juma:Samedi), kwa hiyo tunatakasa siku ya kwanza, si siku ya saba, Jumapili maana yake, na sasa ni, siku ya Bwana.”TSHM 216.4

    Kama alama ya mamlaka ya Kanisa la Wakatoliki, waandishi wa Kanisa la Roma wananena “Tendo kabisa la kugeuza Sabato kwa Jumapili (siku ya kwanza ya juma), ambalo Waprotestanti wanakubali; ... kwa sababu ya kushika Jumapili (siku ya kwanza ya juma), wanakubali mamlaka ya kanisa kwa kuamuru siku kuu, na kuzitawala chini ya zambi.”TSHM 216.5

    Ni nini tena badiliko la Sabato, lakini ni alama, ao chapa, cha mamlaka ya Kanisa la Roma--“chapa ya mnyama”?TSHM 217.1

    Kanisa la Roma halikuacha madai yake kwa mamlaka. Wakati ulimwengu na makanisa ya Waprotestanti wanapokubali sabato iliotungwa na Roma, wakati wanapokataa Sabato ya Biblia, wanakubali kwa kweli majivuno haya. Kwa kufanya vile wanazarau kanuni zinazowatenga kwa Roma--kwamba “Biblia, na ni Biblia tu, ni dini ya Waprotestanti.” Kwa namna mwendo kwa ajili yakulazimisha Jumapili (siku ya kwanza ya juma) unapata upendeleo, mwishoni italeta Waprotestanti wote chini ya bendera ya Roma.TSHM 217.2

    Wakristo wa Kanisa la Roma wanatangaza kwamba “kushika Jumapili (siku ya kwanza ya juma) kwa Waprotestanti ni heshima kuu wanatoa, kwa kujichukia wenyewe, kwa mamlaka ya Kanisa [la Katoliki].”7 Kwa kulazimisha kazi ya dini kwa mamlaka ya serkali ni kufanya sanamu kwa mnyama; kwa hiyo kulazimisha kushika Jumapili (siku ya kwanza ya juma) katika Amerika kungekuwa kulazimusha kuabudu ya mnyama na sanamu yake.TSHM 217.3

    Wakristo wa vizazi vilivyopita walishika Jumapili (siku ya kwanza ya juma) wakizani kwamba walikuwa wakishika Sabato ya Biblia, sasa kunakuwa Wakristo wa kweli katika kila kanisa ambao kwa uaminifu wanaamini kwamba Jumapili (siku ya kwanza ya juma) ni agizo la kimungu. Mungu anakubali uaminifu wao na uhaki yao. Lakini wakati kushika Jumapili (siku ya kwanza ya juma) itakapolazimishwa kwa sheria na ulimwengu utaangaziwa juu ya Sabato ya kweli, ndipo ye yote atakayevunja amri ya Mungu kwa kutii amri ya Roma kwa hiyo atakuwa anaheshimu mafundisho ya kipapa kuliko ya Mungu. Anakuwa akitoa heshima kwa Roma. Anakuwa akiabudu mnyama na sanamu yake. Ndipo watu watapokea chapa cha utii kwa Roma--“chapa ya mnyama.” Yale hayatafanyika hata mambo yanapowekwa wazi mbele ya watu na watakapoletwa kwa kuchagua kati ya amri za Mungu na amri za watu, ndipo wale wanaoendelea katika kuvunja amri watapokea “chapa ya mnyama.”TSHM 217.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents