Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Watu wa Mungu Hawataongozwa Vibaya

    Lakini watu wa Mungu hawataongozwa vibaya. Mafundisho ya kristo huyu wa uwongo hayaako kwa mapatano na Maandiko. Baraka yake itatamkwa juu ya waabuduo wa mnyama na sanamu yake, ni kundi kabisa ambalo Biblia inatangaza ya Kwamba gazabu ya Mungu pasipo kuchanganywa itamiminwa.TSHM 304.2

    Tena zaidi, Shetani hakuruhusiwa kuiga namna ya majilio ya Kristo. Mwokozi ameonya watu wake juu ya madanganyo kwa jambo hili. “Kwa sababu Wakristo wa uwongo watasimama, na manabii za uwongo, nao wataonyesha alama kubwa na maajabu wapate kudanganya kama ikiwezekana, hata wachaguliwa... Basi kama wakiwaambia ninyi: Tazama yeye ni jangwani; musitoke; Tazama, yeye ni katika vyumba vya ndani nyumbani, musisadiki. Kwa maana kama umeme unavyokuja toka mashariki na unaangaza hata mangaribi; hivi kuja kwa Mwana wa watu kutakavyokuwa vile”. Matayo 24:24-27. Utazame vilevile Matayo 25:31; Ufunuo 1:7; 1 Watesalonika 4:16,17. Kuja huku, hapo hakuna namna ya kuiga. Itashuhudiwa kwa ulimwengu wote mzima.TSHM 304.3

    Ila wanafunzi wa juhudi tu wa Maandiko waliokubali upendo wa kweli watakaolindwa kwa madanganyo ya nguvu yanayofanya dunia kuwa mateka. Kwa ushuhuda wa Biblia hawa watavumbua mdanganyi huyu kwa umbo la uwongo wake. Je, watu wa Mungu sasa wanakuwa wenye imara sana kwa Neno lake ili wasingejitoa kwa ushuhuda wa mashauri yao? Je, katika shida ya namna hii, wangeshikamana kwa Biblia, na kwa Biblia pekee?TSHM 304.4

    Wakati watawala wa Kikristo watakapotangaza agizo juu ya wenye kushika amri kuondolewa kwa ulinzi wa serkali na kuwaacha kwa wale wanaotaka maangamizi yao, watu wa Mungu watakimbia kutoka katika miji na vijiji na kushirikiana pamoja katika makundi, kukaa katika mahali pa ukiwa sana na pa upekee. Wengi watapata kimbilio katika ngome za milima, kama Wakristo wa mabonde ya Piedmont (Vaudois). (Tazama sura ya ine). Lakini wengi katika mataifa yote na makundi yote, wa juu na chini, watajiri na maskini, weusi na weupe, watatupwa katika utumwa usio na haki kabisa na wa jeuri. Wapenzi wa Mungu watapitia kwa siku za taabu kufungiwa ndani ya gereza ya fito za chuma, kupewa hukumu ya kuuawa, labda kuachiwa kufa katika giza, gereza la kuchukiza mno.TSHM 305.1

    Je, Bwana atasahau watu wake kwa saa hii ya majaribu? Je, alimsahau muaminifu Nuhu, Loti, Yusufu, Elia, Yeremia, ao Danieli? Ingawa adui wakiwasukuma kwa nguvu katika gereza, lakini kuta za gereza haziwezi kukata habari kati ya nafsi zao na Kristo. Malaika watakuja kwao katika vyumba vya kifungo vya kipekee. Gereza itakuwa kama jumba la mfalme, na kuta za giza zitaangaziwa kama vile Paulo na Sila walipokuwa wakiimba usiku wa manane katika gereza ya Wafilipi.TSHM 305.2

    Hukumu za Mungu zitajia wale wanaotaka kuangamiza watu wake. Kwa Mungu, azabu ni “tendo la kigeni”. Isaya 28:21; utazame vilevile Ezekieli 23:11. Bwana ni mwenye”rehema na mwenye neema, si mwepesi kwa hasira, mwema na kweli nyingi, ... akisamehe uovu na makosa na zambi”. Lakini “hataachilia wenye zambi hata kidogo”. Kutoka 34:6, 7; Nahamu 1:3. Taifa inalostahimili wakati mrefu, na linalojaza kipimo cha uovu wake, mwishoni litakunywa kikombe cha hasira pasipo kuchanganywa na rehema.TSHM 305.3

    Wakati Kristo anapomaliza uombezi wake katika Pahali patakatifu, hasira (ghazabu) pasipo kuchanganywa itahofishwa juu ya wale wanaoabudu mnyama itamiminwa. Mapigo kwa Misri yalikuwa ya namna moja na hukumu zenye eneo kubwa zaidi zile ambazo zinapaswa kuanguka duniani mbele kabisa ya wokovu wa mwisho wa watu wa Mungu. Asema mfumbuzi: “Ikaanguka jipu mbaya, zito, juu ya watu wenye chapa ya mnyama, na wale walioabudu sanamu yake. “Bahari “ikakuwa damu kama damu ya mfu”. Na “mito na chemchemi za maji; zikakuwa damu”. Malaika anatangaza: “Wewe mwenye haki, Bwana, ... kwa sababu umehukumu hivi. Kwani walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu kunywa; nao wamestahili”. Ufunuo 16:2-6. Kwa kuhukumu watu wa Mungu hukumu ya mauti, kwa kweli wamehesabiwa makosa ya damu yao kama ingemwagika na mikono yao. Kristo alitangaza kwa Wayahudi wa wakati wake kosa ya damu yote ya watu watakatifu iliyomwagika tangu siku za Abeli (Matayo 23:34-36). Kwani walikuwa na roho ya namna moja kama wauaji hawa wa manabii.TSHM 305.4

    Kwa pigo linalofuata, uwezo unatolewa kwa jua “kuunguza watu kwa moto”. Ufunua 16:8,9. Manabii wanaeleza wakati huu wakutisha: “Mavuno ya shamba yameharibiwa... miti yote ya shamba imekauka kwa sababu furaha imekauka katika wana wa watu”. “Wanyama wanamlio wa huzuni makundi ya mifungo yanafzaika, sababu nawana malisho.... Maji ya mito yamekauka, na moto umekula malisho ya jangwa”. Joel 1:11,12, 18-20.TSHM 306.1

    Mapigo haya si ya mahali pote, lakini yatakuwa mapigo ya kutisha zaidi isiyofahamika kamwe. Hukumu zote zilizotangulia kufungwa kwa rehema zilikuwa zikichanganyika na rehema. Damu ya Kristo imelinda mwenye zambi kwa kiasi kamili cha kosa lake; lakini kwa hukumu ya mwisho, hasira si ya kuchanganywa na rehema. Wengi watatamani ulinzi wa rehema ya Mungu ambayo walikuwa wakiizarau.TSHM 306.2

    Wakati wanapoteseka na kusumbuliwa, wakati wanapoteseka na njaa, watu wa Mungu hawataachwa kuangamizwa. Malaika watawatolea mahitaji yao. “Atapewa chakula chake; maji yake hayatakosekana”. “Mimi, Bwana, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha”. Isaya 33:16; 41:17.TSHM 306.3

    Lakini kwa maonyo ya kibinadamu itaonekana ya kwamba watu wa Mungu wangepashwa upesi kutia muhuri kwa ushuhuda wao kwa damu yao, kama walivyofanya wafia dini mbele yao. Ni wakati wa maumivu makuu ya kutisha. Waovu wameshangilia. “Imani yenu inakuwa wapi sasa? Sababu gani Mungu hawaokoi kwa mikono yetu kama munakuwa kweli watu wake”? Lakini wanaongojea wanakumbuka Kristo alipokufa juu ya msalaba wa Kalvari. Kama Yakobo, wote wanashindana na Mungu.TSHM 306.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents