Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Habari Njema Imetolewa kwa Ulimwenguni

    “Naye ataimarisha na wengi muda wa juma moja” mwisho wa miaka saba ya mda uliogawanywa kwa Wayahudi. Kwa wakati huu, kutoka kwa mwaka 27 A.D. hata A.D. 34, Kristo na wanafunzi wake wakaeneza mwaliko wa Habari Njema zaidi kwa Wayahudi. Agizo la Mwokozi lilikuwa: “Musiende katika njia ya Mataifa, wala musiingie mji wo wote wa Wasamaria; lakini zaidi kwendeni kwa kondoo wapotevu za nyumba ya Israeli.” Matayo 10:5, 6.TSHM 156.1

    “Na kwa nusu ya juma atakomesha sadaka na toleo.” Katika mwaka A.D. 31,miaka tatu na nusu baada ya ubatizo wake, Bwana wetu alisulibishwa. Kwa kafara kubwa iliyotolewa kule Golgota, mfano ukakutana na kilicho asili ya mfano. Kafara zote na sadaka za kawaida za ibada zilipashwa kukomeshwa.TSHM 156.2

    Miaka 490 iliyogawanyiwa kwa Wayahudi ikamalizika katika mwaka A.D. 34. Kwa wakati ule, kwa njia ya tendo la Baraza (Sanhedrin) la Wayahudi, taifa likatia mhuri wa kukataa injili kwa kifo cha Stefano na mateso ya wafuasi wa Kristo. Ndipo ujumbe wa wokovu ukatolewa ulimwenguni. Wanafunzi wakalazimishwa na mateso kukimbia toka Yerusalema, “wakakwenda pahali po pote wakihubiri neno.” Matendo 8:4.TSHM 156.3

    Kwa hiyo maelezo yote ya mambo ya unabii yakatimia kwa ajabu sana. Mwanzo wa majuma makumi saba ukaimarishwa bila swali lo lote kwa mwaka 457 B.C., na kumalizika kwayo katika mwaka A.D. 34. Majuma makumi saba (siku 490) kukatwa kutoka kwa 2300, hapo kulikuwa siku 1810 zilizobakia. Baada ya mwisho wa siku 490, siku 1810 zilipashwa kutimia. Kutoka A.D. 34, miaka 1810 ikafika kwa mwaka 1844. Kwa hiyo siku 2300 za Danieli 8:14 zikamalizika katika 1844. Kwa kumalizika kwa mda kubwa huu wa unabii, “Pahali patakatifu patasafishwa”--ambaye wafafanisi wengi zaidi wanachanganya na kuja kwa mara ya pili--kukaimarishwa. (Tazama chart, p. 220.)TSHM 156.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents