Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mungu wa Kike wa Kutumia Akili

    “Kusimamisha Mungu wa Kike wa Kutumia Akili kukafanywa upya na kuigwa na taifa po pote, katika mahali ambapo wakaaji walitaka kujionyesha wenyewe kulingana na usitawi wote wa Mapinduzi.”TSHM 129.2

    Wakati “mungu wa kike” alipoletwa kwa Mapatano; msemaji akamkamata kwa mkono, na akageukia makutano akasema: “Wanadamu, muache kutetemeka mbele ya ngurumo zaifu za mungu ambazo wogo wenu umezifanya. Tangu leo msikubali tena umungu mwengine bali Kutumia Akili. Ninawapongoatia picha yake bora na safi sana; kama kunapaswa kuwa na sanamu, mjitoe tu kwa hii. ...TSHM 129.3

    “Mungu wa kike alipokwisha kukumbatiana na msimamizi, akapandishwa kwa gari tukufu kabisa, na akapelekwa kwa kanisa kubwa la Notre Dame, kupata nafasi ya Umungu. Hapo akainuliwa kwa mazabahu ya juu, na kuabudiwa na wote waliokuwako.”TSHM 129.4

    Dini ya Papa alianza kufanya kazi ambayo kukana Mungu kulikuwa kukitimiza, kuharakisha Ufransa kwa uharibifu. Waandishi kwa kutaja machukizo ya Mapinduzi wakasema kwamba mazidio haya yalipaswa kuwekwa juu ya kiti cha mfalme na kanisa. (Tazama Nyongezo.) Kwa haki yote, mazidio haya inapaswa kuwekwa juu ya kanisa. Kanisa la Papa lilipotosha mafikara ya wafalme juu ya Matengenezo. Ujanja wa Roma ilisababisha ukali na ugandamizi kutoka kwa uliotumiwa mamlaka ya mfalme.TSHM 129.5

    Po pote injili ilikubaliwa, mafikara ya watu yakaamshwa. Wakaanza kutupa minyorori (viungo vya pingu vilivyowashikilia) kuwa watumwa wa ujinga na ibada ya sanamu. Wafalme waliviona na wakatetemeka kwa ajili ya uonevu wao.TSHM 130.1

    Roma ikaharakisha kuwasha vitisho vyao vya wivu. Katika mwaka 1525, Papa akasema kwa watawala wa Ufransa: “Huyu wazimu shetani (Dini ya Kiprotestanti) hatatoshelewa kuchafua dini na kuiangamiza, bali mamlaka zote, cheo kikubwa, sheria, amri, na hata madaraja tena.” Tangazo la Papa likaonya mfalme: “Waprotestanti watapindua amri yote ya serkali na ya dini pia. ... Kiti cha mfalme kinakuwa hatarini kama vile mazabahu.” Roma ikafaulu kupanga Ufransa kwa kupinga Matengenezo.TSHM 130.2

    Mafundisho ya Biblia yangeimarisha katika mioyo ya watu kanuni za haki, kiasi, na kweli, vinavyokuwa jiwe la pembeni kwa usitawi wa taifa. “Haki inainua taifa.” Maana “Kiti cha ufalme kinasimamishwa kwa haki.” Mezali 14:34; 16:12. Tazama Isaya 32:17. Yeye anayetii sheria ya Mungu atazidi kwa kweli kuheshimu na kutii amri za inchi. Ufransa ulikataza Biblia. Karne kwa karne watu wa haki, wa ukamilifu wa elimu na matendo mema, waliokuwa na imani kwa kuteseka kwa ajili ya kweli, wakaenda kwa taabu kama watumwa katika jahazi, wakaangamizwa kwa kigingi (tita), ao kuoza ndani ya pango za gereza. Maelfu wakapata usalama katika kukimbia kwa miaka 250 baada ya kufunguliwa kwa Matengenezo.TSHM 130.3

    “Labda hapakuwa na kizazi cha Ufransa, kwa mda wa wakati ule mrefu ambao hawakushuhudia wanafunzi wa injili kukimbia mbele ya mauaji kali ya wazimu ya watesi wao, na kuchukua akili yao pamoja nao, vitu vya ufundi, utendaji, na roho yao ya utaratibu, kwa kutangulia wakapita, kwa kutayarisha inchi ziiizowapatia kimbilio. ... Kama hawa wote sasa waliofukuza wangalirudi Ufransa, ingalikuwa inchi ya namna gani ... kubwa, ya usitawi, na ya furaha--mfano kwa mataifa--ingalikuwa! Lakini bidii isiyo ya akili ya upofu na kizazi kisichokuwa na huruma kikafukuza kwa inchi yake kila mwalimu wa nguvu, kila shujaa wa roho ya utaratibu, kila mtetezi mwaminifu wa kiti cha mfalme. ... Mwishowe uharibifu wa taifa ukatimilika.”TSHM 130.4

    Matokeo yake yalikuwa Mapinduzi pamoja na machafuko.TSHM 130.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents