Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    42 / AMANI YA MILELE: VITA IMEMALIZIKA

    Kwa mwisho wa miaka 1000, Kristo anarudi duniani akisindikizwa na waliokombolewa na jamii ya malaika. Anaagiza wafu waovu watoke kupokea maangamizi yao. Wanatoka, wengi sana kama mchanga wa bahari, wanapokuwa na alama za ugonjwa na mauti. Tofauti namna gani kwa wale waliofufuka katika ufufuko wa kwanza!TSHM 323.1

    Macho yote inageuka kutazama utukufu wa Mwana wa Mungu. Kwa sauti moja majeshi ya waovu wanapaza sauti: “Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana”! Matayo 23:39. Si mapendo yanayoongoza maneno haya. Nguvu ya kweli inalazimisha maneno kutoka kwa midomo isiyotaka. Kama vile waovu walivyokwenda katika makaburi, ndivyo hivyo wanafufuka pamoja na uadui wa namna moja kwa Kristo na roho ya namna ileile ya uasi. Hawatapewa wakati wa rehema mpya kwa kuponyesha maisha yao ya wakati uliopita.TSHM 323.2

    Nabii anasema: “Na miguu yake itasimama siku ile juu ya mlima wa Mzeituni, ... na Mlima wa Mzeituni utapasuka katikati yake”. Zakaria 14:4. Wakati Yerusalema mpya unaposhuka toka mbinguni, utapumzika kwa pahali palipotayarishwa, na Kristo, pamoja na watu wake na malaika, wanaingia kwa mji mtakatifu.TSHM 323.3

    Wakati alipokatwa kazi yake ya kudanganya, mtawala wa uovu alikuwa maskini na mwenye huzuni, lakini kwa namna wafu waovu wanapofufuka na anapoona makutano makubwa kwa upande wake, matumaini yake yanarudi. Anakusudia si kutokuacha vita kubwa. Atapanga wapotevu chini ya bendera yake. Kwa kukana Kristo wamekubali amri ya mwongozi mwasi, tayari kufanya mapenzi yake. Lakini, kweli kwa werevu wake wa kwanza, hakubali yeye mwenyewe kuwa Shetani. Anadai kuwa mwenyewe wadunia wa haki ambaye alinyanganywa uriti bila sheria. Anajionyesha mwenyewe kama mkombozi, kuhakikisha watu wake waliodanganyiwa ya kwamba uwezo wake umewaleta kutoka kwa makaburi yao. Shetani anawafanya wazaifu kuwa wenye nguvu, na kuwasukuma wote kwa nguvu zake mwenyewe kuwaongoza kukamata makao ya mji wa Mungu. Akatazama kwa mamilioni yasiyohesabika ya waliofufuliwa kutoka kwa wafu, na akatangaza ya kwamba kama muongozi wao anaweza kupata tena kiti chake chaenzi na ufalme.TSHM 323.4

    Katika makutano makubwa haya kunakuwa na taifa lenye maisha marefu lile lililoishi mbele ya garika, watu wa kimo kirefu sana na wa akili nyingi; watu ambao kazi zao za ajabu zikaongoza ulimwengu kuabudu akili zao, lakini mambo ya uvumbuzi wa ukali na uovu wao ikafanya Mungu kuwaharibu kutoka kwa viumbe vyake. Pale kunakuwa wafalme na wajemadari wasioshindwa kamwe kwa vita. Katika mauti hawa hawakupata badiliko. Wanapotoka kwa kaburi, wanaendeshwa kwa tamaa ya namna ileile ya kushinda wale waliowatawala wakati walishindwa.TSHM 323.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents