Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    22 / UNABII UNATIMILIKA

    Wakati ulipopita ambapo kuja kwa Bwana kulipotazamiwa kwanza--wakati wa masika ya mwaka 1844--wale waliotazamia kuonekana kwake walikuwa katika mashaka na kutokuwa na hakika. Wengi wakaendelea kuchunguza katika Maandiko, kwa kupima tena ushuhuda wa imani yao. Maneno ya unabii, ya wazi na ya nguvu, yalionyesha kuja kwa Kristo kuwa karibu. Kugeuka kwa waovu na uamsho wa kiroho miongoni mwa Wakristo kulishuhudia kwamba ujumbe ulikuwa wa mbinguni. Walihangaishwa na mambo ya unabii, ambayo walizania kama, kulingana na wakati wa kuja kwa mara ya pili, ilikuwa fundisho la kuwatia moyo kwa kungoja na uvumilivu katika imani,ili mambo yaliokuwa giza kwa akili yao sasa ifunuliwe. Miongoni mwa mambo haya ya unabii ilikuwa Habakuki 2:1-4. Hakuna mtu, hata, aliyefahamu kwamba kukawia kwa wazi--wakati wa kungojea--unakuwa katika unabii. Baada ya uchungu, andiko hili likaonekana kuwa la maana sana: “Maono haya ni kwa wakati ulioamuriwa, lakini kwa mwisho yatasema, wala hayatasema uwongo; hata yakikawia, uyangoje; kwa sababu yatakuja kweli, hayatachelewa. . . Mwenye haki ataishi kwa imani yake.”TSHM 188.1

    Unabii wa Ezekieli pia ulikuwa faraja kwa waaminifu:TSHM 188.2

    “Bwana Mungu anasema hivi... Siku ni karibu, na kutimia kwa kila maono ... Nitasema, na neno nitakalolisema litatimizwa; wala halitakawishwa tena.” “Neno nitakalolisema litatimia.” Ezekieli 12:2325,28.TSHM 188.3

    Wale waliokuwa wakingoja wakafurahi. Yeye anayejua mwisho tangu mwanzo aliwapa tumaini. Kama mafungu kama haya ya Maandiko hayangekuwako, imani yao ingalianguka.TSHM 188.4

    Mfano wa mabikira kumi wa Matayo 25 pia unaonyesha mambo ya maisha ya Waadventiste. Hapo paonyeshwa hali ya kanisa wakati wa siku za mwisho. Mambo yao ya maisha yamefananishwa na tendo la ndoa ya mashariki:TSHM 188.5

    “Halafu ufalme wa mbinguni utafananishwa na mabikira kumi waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kukutana na bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbafu na watano wenye akili. Wale walio kuwa wapumbafu, walichukua taa zao, bila mafuta; lakini wenye akili walicukua mafuta ndani ya vyombo vyao pamoja na taa zao. Basi wakati bwana arusi alipokawia, wao wote wakasinzia na kulala usingizi. Lakini saa sita ya usiku kulikuwa kelele: Tazama, bwana arusi! tokeni kukutana naye.” Matayo 25:1-6.TSHM 188.6

    Kuja kwa Kristo kama kulivyotangazwa na ujumbe wa malaika wa kwanza, kulifahamika kuwa mfano wa kuja kwa bwana arusi. Kuenea kwa matengenezo chini ya kutangaza kwa kuja kwa karibu kwa Kristo kukajibu kwa mfano wa mabikira. Katika mfano huu, wote walichukua taa zao, Biblia, “na wakaenda kukutana na bwana harusi.” Lakini wakati wapumbafu “hawakuchukua mafuta pamoja nao,” “wenye akili walichukua mafuta ndani ya vyombo vyao pamoja na taa zao.” Wa nyuma wakajifunza Maandiko ili kuchunguza ukweli na wakawa na akili ya kipekee, imani kwa Mungu ambayo haingeangushwa na kukata tamaa na kukawia. Wengine wakaendeshwa na musukumo, hofu yao ikaamshwa na ujumbe. Lakini imani yao ilijengwa juu ya imani ya ndugu zao, walitoshelewa na nuru yenye kuwayawaya ya maono, bila ufahamu kamili wa kweli wala kazi halisi ya neema ndani ya moyo. Hawa wakaendelea “kukutana” na Bwana katika matazamio ya zawadi ya mara moja lakini hawakutayarishwa kwa kukawia na uchungu. Imani yao ikaanguka.TSHM 189.1

    “Wakati bwana arusi alipokawia, wao wote wakasinzia na kulala usingizi.” Kwa kukawia kwa bwana arusi ni mfano wa kupitisha wakati, kukata tamaa, ni kukawia kwenye kuonekana kwa inje. Wale ambao imani yao iliimarishwa juu ya ujuzi wa kipekee wa Biblia walikuwa na mwamba chini ya miguu yao ambayo mawimbi ya uchungu hayakuweza kuharibu. “Wao wote wakasinzia na kulala usingizi,” kundi moja katika kuacha imani yao, lingine likangoja kwa uvumilivu hata mwangaza wazi zaidi ulipaswa kutolewa. Wale wa kijuujuu hawakuweza tena kuegemea kwa imani ya ndugu zao. Kila mmoja anapaswa kusimama ao kuanguka yeye mwenyewe.TSHM 189.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents